Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maofisa watano na watumishi watatu wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 80.
Akizungumza na viongozi wa mamlaka ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA,katika ziara ya kushtukiza leo,Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu wa TRA,Rished Bade na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA,Lusekelo Mwasena,wahakikishe wanashirikiana na polisi kufuatilia upotevu huo na na kwamba fesha hizo zinapatikana na zinarudi Serikalini.
Akitangaza uamuzi huo baada ya kufanya kikao na viongozi wa Serikali bandarini hapo,Waziri Mkuu aliwataja waliosimamishwa kazi kuwa ni Kamishna wa forodha,Tiagi Masamaki na mkuu wa kituo cha huduma kwa wateja, Habibu Mponezya.
“IGP,Ninaagiza watu hawa wakamatwe na kuisaidia polisi,hati zao za kusafiria zikamatwe na mali zao zikaguliwe kama zinaendana na utumishi wa umma,”alisema Waziri Mkuu.
Watumishi wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA,Haruni Mpande,Hamisi Ali Omari(hakutaja anatoka kitengo gani)pamoja na mkuu wa kitengo cha Bandari Kavu (ICD In –Charge),Eliachi Mrema na alitaka wawe chini ya polisi lpaka uchunguzi utakapokamilika.