Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Monday, May 28, 2018

KINANA, MBUYU KWENYE MSITU WA SIASA

Image may contain: 2 people, people smiling, people standing
Na Emmanuel J. Shilatu

Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Abdulrahman Omar Kinana anatajwa kuwa katika orodha ya safu za viongozi mibuyu na migude kwenye misitu minene ya siasa yenye kuhimili tufani za kila aina pia Mwanasiasa anayependa kuheshimu utamaduni, utaratibu na mwenye kuishi kwa misingi ya nidhamu .

Kinana anatajwa kama zao miongoni mwa kunga zitokanazo na mazao katika medani za siasa, utawala, uongozi na aliyeshiba ujuzi toshelezi wa masuala ya diplomasia ya siasa pia anayejua mahusiano yatokanayo na historia, harakati za ukombozi na umoja wa Afrika.

Sauti yake aghalabu huwa na mvumo wa mawimbi ya busara, fikara njema na hekima zenye wito pele aamuapo kusema, kukosoa, kutetea, kukumbusha, kushauri au kuonya kutokana na tabia yake ya kufanya yote hayo kwa hali ya kujiamini akiwa na nguvu ya hoja.

Ukimya wa Mwanasiasa huyo siku zote ni kama mfano wa Simba hodari awindae nyikani au mbugani akiwa hana pupa wala kiherehere. Huyafanya yote kwa utulivu na umakini mkubwa ambao baadae haumletei majuto, athari wala taathira.

Ni Mwanasiasa wa aina yake aliyewahi kuhitajiwa na Marais (Wenyeviti) watatu awe katibu mkuu wa CCM akakataa huku akitoa madai mazito yenye msingi, nguvu ya hoja na maana.



Thursday, May 24, 2018

MAPORI MATANO YA AKIBA MKOANI KAGERA NA GEITA KUPANDISHWA HADHI YA KUWA HIFADHI ZA TAIFA


PICHANI: Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza bungeni alipokuwa akijibu hoja wa wabunge waliochangia mjadala wa bajeti wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma juzi.

Na Mwandishi Wetu

Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza kuanza mchakato wa kuyapandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Burigi, Kimisi, Biharamulo, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa. Mchakato huo tayari umeungwa mkono na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Hayo yameelezwa juzi bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akihitimisha mjadala wa bajeti wa makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

“Mheshimiwa Spika, ninaomba kulitaarifu Bunge lako tukufu kuwa Mhe. Rais ameridhia ombi letu la kupandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Burigi, Kimisi, Biharamulo, Ibanda na Chief Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa, kipekee namshukuru sana Mhe. Rais kwa kuridhia ombi letu hilo” amesema Dkt. Kigwangalla.

Amesema kufuatia hatua hiyo, wizara yake inaanzisha mchakato rasmi wa kukamilisha taratibu za kupandisha hadhi mapori hayo ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii katika kanda ya Kaskazini Magharibi na hivyo kufikia azma ya Serikali kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni 8 na mapato ya dola za kimarekani bilioni 16 katika kipindi cha miaka 7 ijayo.

Inaelezwa kuwa mchakato huo utapitia hatua mbalimbali ikiwemo kuwashirikisha wadau husika kupata maoni yao, mapendekezo kuwasilishwa baraza la mawaziri kabla ya kujadiliwa bungeni na hatimaye kuwasilishwa kwa Mhe. Rais kwa ajili ya kuidhinishwa kuwa Sheria kamili ya kupandisha hadhi mapori hayo.



Monday, May 21, 2018

SERIKALI YAHIMIZA HALMASHAURI KUBUNI MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUJIONGEZEA MAPATO

PICHANI: Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akijibu maswali Bungeni, Jijini Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Uchukuaji wa baadhi ya vyanzo vya mapato katika halmashauri ulifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti iliyoridhiwa na Bunge ya mwaka 2015 kifungu namba 58 ikiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa ukusanyaji na matumizi ya mapato hayo.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Suzana Mgonukulima, aliyependekeza itungwe sheria ya kuibana serikali ikiwa haitarejesha fedha zilizotokana na vyanzo vya mapato vilivyopo kwenye Miji, Halmashauri, Manispaa na Majiji zitakazokusanywa na kuwekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Bajeti, mgao wa fedha kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali utazingatia bajeti iliyoidhinishwa, upatikanaji na mtiririko wa fedha, utekelezaji mpango wa ununuzi na mpango wa kuajiri hivyo hakuna Fungu litakaloruhusiwa kufanya matumizi ya aina yoyote mpaka kuwe na fedha za kulipa matumizi husika.



RITTA KABATI CHALLENGE CUP MSIMU 2018 YAANZA RASMI,TIMU ZAOMBWA KUCHUA FOMU KUSHIRIKI


Kulia ni Mwenyekiti wa mashindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 na kushoto ni katibu wa kamati ya mshindano hayo walipokuwa wakiongea na vyombo vya habari kwenye ofisi zao zilizopo manispaa ya Iringa mkoani Iringa mapema hii leo


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Kamati ya ya mshindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 imezindua rasmi kwa kuanza kuzialika timu kwa ajiri ya kuchukua fomu kushiriki na wameweka bayana jinsi mfumo wa mashindano utakavyokuwa pamoja na zawadi kwa washindi wote.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa mashindano hayo Gerald Malekela alisema kuwa analialika timu mbalimbali za mkoa wa Iringa kuja kuchukua fomu za mashindano kwa gharama ya shilingi elfu thelathini (30,000/=) ambazo zinapatikana katika kituo cha radio cha Nuru Fm.

“Naomba viongozi wa vilabu vinavyotaka kushiriki mashindano haya vinatakuwa kufika katika ofisi za Nuru fm au kumpigia mratibu wa mashindano haya Fredy Mgunda kwa kumpigia simu ya nambari 0714201006 au mnipigie mimi mwenyewe kwa namba hii 0762687732 hapo utakuwa umerahisisha jinsi ya kuzipata hizo fomu na maelezo kwa kina” alisema Malekela



Wednesday, May 16, 2018

KAND YA ZIWA VICTORIA WAKOSOA VIKALI TABIA YA WANASIASA KUIPAKA MATOPE SERIKALI VITA UVUVU HARAMU


PICHANI : Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akihutubia hadhara ya kikosi kazi cha watu 260 alichokiunda kwa ajili ya operesheni Sangara 2018 na Wakuu wa Mikoa mitano inayozunguka Ziwa vicktoria wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni hiyo. Picha na John Mapepele

NA JOHN MAPEPELE, MWANZA

WAKUU wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria wamekosoa vikali tabia ya baadhi ya wanasiasa kuipaka matope dhamira njema ya Serikali ya kupambana na uvuvi haramu ulioshamiri katika ziwa hilo na kutaka viongozi wa aina hiyo kutangaza masilahi yao kwenye eneo la uvuvi kabla ya kuwashambulia viongozi wanaosimamia zoezi hilo kwa misingi ya kisheria.

Wakizungumza kwenye kikao cha tathmini ya operesheni sangara awamu ya pili iliyowahusisha Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Makamanda wa Polisi wa mikoa na Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa wa mikoa yote inayozunguka Ziwa Victoria jijini Mwanza jana viongozi hao wametaka hatua zaidi zichukuliwe ili kunusuru rasilimali hizo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka alielezea kuchukizwa na tabia inayoanza kuota mizizi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuipaka matope dhamira nzuri ya Serikali ya kukabiliana na uvuvi haramu na kutaka viongozi wa aina hiyo watangaze masilahi yao kabla ya kuanza kuwashambulia viongozi wanaosimamia operesheni hiyo inayotekelezwa kwa mujibu wa sheria .

“Viongozi wanaopinga operesheni ya kupambana na uvuvi haramu ni muhimu watangaze kwanza masilahi yao kuhusu eneo la uvuvi ili wasiendelee kuchafua taswira za viongozi wanaosimamia wizara hii”alisema Mtaka.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema kumekuwepo na dhana zinazojengeka kwamba viongozi wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria hawaungi mkono mapambano ya kukabiliana na uvuvi haramu operesheni jambo ambalo alisema ni upotoshaji mkubwa na kwamba Serikali ya mkoa iko mstari wa mbele na kuwabana watendaji wa ngazi zote watakaobanika kufadhili uvuvi haramu.



Monday, May 14, 2018

WAZIRI UMMY AZINDUA TAWI LA CCM KATA YA USAGARA APOKEA WANACHAMA 50

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Malumu (CCM) mkoa wa Tanga akimkabidhi kadi ya CCM moja ya wanachama wapya waliojiungana chama hicho wakati alipokwenda kufungua tawi la CCM Kata ya Usagara

leo ambapo jumla ya wanachama wapya 50 walipokelewa kulia ni Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini (CCM) Joseph Msukuma





Sunday, May 13, 2018

SERIKALI - HAKUTAKUWA NA UPUNGUFU WA SUKARI


PICHANI : Waziri wa Kilimo na Ushirika,  Mhe. Dkt. Charles Tizeba

Serikali imeagiza sukari kiasi cha tani 70,354.35 kutoka nchi za nje lengo likiwa ni kujipanga ili kuhakikisha kuwa hapatokei upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni waziri wa kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa tani 60,539.35 ya sukari itaanza kuingia hapa nchini katikati ya mwezi Mei 2018 ambapo kiasi kilichobaki cha tani 9,815 kitaingia mwezi June mwaka 2018.

Aidha Dkt. Tizeba amefafanua kwamba hakutarajiwi kuwa na upungufu wa sukari hapa nchini kwa sababu hadi kufikia tarehe 10 mei 2018 katika maghala ya wazalishaji na wafanyabiashara kulikuwa na tani 78,147.67 za sukari na kiasi kingine tani 25,441.25 kipo Bandarini .

Kwa kiasi cha sukari ambacho tayari kipo hapa nchini kikijumlishwa na kiasi ambacho kitaingia hivi karibuni kutoka nje ya nchi ni dhahiri kwamba nchi haiwezi kupata upungufu wa bidhaa hiyo, alisema Mhe.Waziri.



Friday, May 04, 2018

RAS TANGA AWAFUNDA WAANDISHI WA HABARI TANGA


PICHANI: Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambayo ilifanyika kimkoa kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa Habari Jijini Tanga kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Edward Bukombe na kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (Tanga Presse Club) Hassan Hashim


WAANDISHI wa Habari Mkoani Tanga wametakiwa kuwajibika kwa kufanya kazi kwa kufuata miongozo na maadili ikiwemo kuweka uzalendo mbele kwa ajili ya maslahi ya nchi na jamii zinazowazunguka.

Hayo yalisemwa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi wakati akizungumza katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambayo ilifanyika kimkoa kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa Habari Jijini Tanga.

Alisema iwapo watazingatia maadili na kuweka mbele uzalendo itasaidia kuweza kuwasaidia kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi na maendeleo kupitia vyombo vya habari ili viweze kupata mafanikio makubwa.

“Ndugu zangu niwaambie uhuru wa habari ukitumika vyema vyombo vya habari vina mchango mkubwa kwa mkoa na nchi katika nyanja za kijamii, kiasiasa na kiuchumi kwa kujenga jamii yenye kiu ya kuleta maendeleo “Alisema.



Sunday, April 15, 2018

WAZIRI MHAGAMA AFUNGUA MKUTANO WA KUTEKELEZA BORA SHERIA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI




  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA

SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama mjini Dodoma mwishoni Aprili 13, 2018, wakati akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma) na Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mhe. Waziri alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.



Friday, March 23, 2018

VITA YA BIASHARA YA CHINA NA MAREKANI KULETA MAAFA YA KIUCHUMI DUNIANI


PICHANI : Rais wa Marekani, Donald Trump akiwa amezungukwa na wafanyabiashara pamoja na maafisa wa wa nchi hiyo, akijiandaa kutia saini taarifa itakayopitisha mpango wa kutoza faini bidhaa za China, katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Washington, Marekani. (Reuters)

Na Mwandishi Wetu wa Kimataifa,
Immamatukio Blog.

China imeitaka Marekani kuachana na malengo yake wakati Rais Trump akiandaa mpango wa kutoza ushuru mpaka kufikia dola bilioni 60 (sawa na shilingi trilioni 135.5 za Tanzania) bidhaa za China, jambo ambalo linaonesha dalili ya vita ya biashara baina ya mataifa hayo makubwa kiuchumi duniani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Rauters, kuongezeka kwa mvutano baina ya Beijing na Washington kumeleta wasiwasi katika masoko ya fedha ambapo wawekezaji wanabashiri matokeo mabaya ya kiuchumi duniani kama patatokea vikwazo vya kibiashara.

Trump anapanga kutoza kodi katika kile utawala wake unachokiita kukosekana kwa usawa katika hatimiliki za Marekani. Uchunguzi ulianza mwaka jana chini ya kifungu 301 cha mwaka 1974 cha Sheria ya Biashara ya Marekani.

“China haitarajii kuingia katika vita ya biashara, lakini haiogopi kupambana” taarifa ya Wizara ya Biashara China ilijibu. China inatumaini Marekani itajitoa katika hatua hiyo na kufanya uamuzi sahihi ili kuondoa hatari za uhusiano”



TANZANIA NA CHINA KUSHIRIKIANA KUONGEZA TIJA UZALISHAJI MAHINDI MOROGORO


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin, akimuonyesha Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, moja ya picha katika Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini, katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji hicho. Mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro na Chuo hicho Kikuu cha Kilimo cha China. Nyuma yao ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro.


 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, akisalimiana na Profesa Wu Jiu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.



UINGEREZA NAYO YAVUNJA MKATABA NA KAMPUNI ILIYOKOSA TENDER YA PASSPORT TANZANIA

PICHA JUU: Muonekanao wa E-Passport zilizotolewa mapema mwaka huu.


PICHANI KUSHOTO: Passport ya Uingereza ambayo kampuni ya De La Rue ilikuwa inazitenegeneza kabla ya kufutiwa mkataba wao.

Na Mwandishi Wetu.

KAMPUNI ya De La Rue ambayo ilishindwa kwenye zabuni ya E-Imigration ambapo ingetengeneza e-passport, e-Visa, e-Imigration nchini Tanzania imepata pigo jingine baada ya mkataba wake kusitishwa na Serikali ya Uingereza ya kuendelea kutengeza hati za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Aliance News imesema kuwa kampuni ya De La Rue ilikuwa na mkataba na Uigereza wa miaka 10 lakini nchi hiyo imeamua kuvunja mkataba kati yake na kampuni hiyo. Imefahamika lengo la Serikali ya Uingereza kuvunja mkataba huo wa kutengenezwa hati za kusafiria ni kutokana na gharama kuwa kubwa za utengenezaji wa hati hizo na hivyo kuamua kuipa zabuni kampuni ya French firm Gemalto.

"Hati mpya za kusafiria za Uingereza hazitatengenezwa tena na kampuni ya De La Rue ambayo ndio iliyotengeneza hati zitumikazo kwa sasa. "Hivyo hati hizo mpya za rangi ya blue ambazo zitatumika baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya zitatengenezwa na kampuni ya French firm Gemalto.

Kubadilika kwa rangi ya hati hiyo kunatafsiriwa kuwa ni alama ya kurudi kwa nguvu ya Uingereza, umesema mtandao uliotoa taarifa hizi. Pia taarifa zinaeleza kuwa Kampuni ya De La Rue inafikiria kukata rufaa baada ya kukosa na kushindwa katika zabuni ya kutengeneza hati hizo mpya. Kampuni hiyo imeripotiwa ikidai haikuridhishwa kwa kupoteza zabuni hivyo hivyo inaweza kukata rufaa kutokana na uamuzi huo wa Serikali ya Uingereza.




Thursday, March 22, 2018

MALAWI YAVUTIWA NA MATIBABU YA KIBINGWA MOI


Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Malawi Dkt. Charles Mwansambo ametembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ili kupata uzoefu wa namna Taasisi hiyo inavyotoa huduma za kibobezi (super specialist).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo leo Jijini Dar es Salaam Dkt. Mwansambo amesema ametembelea MOI ili kuona uwezekano wa kuwaleta wagonjwa wa Malawi kupata huduma za Kibingwa za Mifupa, Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu badala yakuwapeleka India.

" Nimefurahi kuona kuwa tuna huduma nzuri za kibingwa kwa jirani zetu wa Tanzania, hili ni jambo jema na litatupunguzia gharama za kuwapeleka wagonjwa India badala yake tunawaleta hapa MOI" amesema Dkt.Mwansambo.

Aidha, Dkt. Mwansambo alipata fursa ya kutembelea vyumba vya upasuaji vya MOI, vyumba vya wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU), wodi za watoto na wodi maalum za kisasa za kulipia.



Wednesday, March 21, 2018

UWT WATEMBELEA KIGABONI, TEMEKE, WAPONGEZA RAIS KUKTANA NA WAFANYABIASHARA


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave akizungumza na Wajumbe Wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Kigamboni, alipofanya ziara ya Kikazi katika Wilaya hiyo na Temeke, leo. Dorothy ambaye alifuatana na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT mkoa huo, amesisitiza kuwa ni lazima viongozi watambue kuwa muda wa maandalizi ya ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao ni sasa.


Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga akizungumza wakati wa kikao cha Kazi kati ya Mwenyekiti wa UWT mkoa huo na Wajumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT Wilaya ya Kigamboni, leo. Malyaga amesema UWT mkoa wa Dar es Salaam, Wanampongeza Rais Dk. John Magufuli kwa uthubutu aliofanya mwishoni mwa wiki iliyopita, kukutana na kufanya mazungumzo ya kina na Wafanyabiashara mbalimbali hapa nchini. "Sisi tunaaamini hatua hii itasaidia sana kuondoa au kupunguza changamoto zinazonyemelea sekta ya biashara nchini", alisema Tatu Malyaga



Tuesday, March 20, 2018

ALIYEKUWA RAIS WA UFARANSA AKAMATWA KWA KUPOKEA HELA ZA GADDAFI 2007

Aliyekuwa rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy (Pichani) amekamatwa na anashikiliwa na polisi akihojiwa kuhusiana na tuhuma za kupokea euro milioni 5 (sawa na Shilingi Bilioni 13.9) kwaajili ya kampeni mwaka 2007 kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.

Ufaransa ilifungua uchunguzi mwaka 2013 zikidai ushindi wa Sarkozy wa mwaka 2007 ulitokana na fedha zisizo halali kutoka kwa Marehemu Gaddafi.

Rafiki wa Sarkozy ambaye pia alikuwa waziri, Brice Hortefeux, naye pia amehojiwa na polisi jumanne asubuhi kuhusiana na uchunguzi huo, chanzo kingine kilichopo karibu na uchunguzi huo kileleza.

Sarkozy, alitawala Ufaransa kuanzia mwaka 2007 mpaka 2012, mar azote amekuwa akikanusha madai ya kufanya kampeni chafu na kupokea kiasi hicho cha fedha kwaajili ya kampeni na kuziita tuhuma hizo “za ajabu”

Mwezi januari mfanyabiasha wa Ufaransa aliyedaiwandiye aliyefikisha fedha hizo ili kufadhili kampeni za Sarkozy toka kwa Gaddafi, alikamatwa nchini Uingereza na kutoka kwa dhamana baada ya kufikishwa katika mahakamani jijini London.

Sarkozy ameshasimamishwa mahakamani kwa tuhuma kama hizo kuhusiana na ufadhili wa kampeni katika uchaguzi wa mwaka 2012 na kushindwa na Francois Hollande.

WATANZANIA WAISHIO WASHINGTON DC NA JUMUIYA MPYA 2018

Siku ya Jumapili March 18, katika ukumbi wa Mount rainier, Maryland, Team Libe walifanikisha azama juu ya mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Jumuiya Mpya ya Watanzania waishio DMV utakaofanyika siku ya Jumapili March 24, 2018


MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MASUALA YA AFYA

PICHANI: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa kimataifa wa masuala ya Afya, uliohudhuliwa na Mawaziri kutoka nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini.

Na WAMJW. 
Dar es salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaaliwa afungua Mkutano wa 65 wa Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, (ECSA HC)

Katika ufunguzi huo Waziri Mkuu amewataka wananchi wanachama wa Jumuiya hiyo kufuata mtindo bora wa maisha pamoja na kufanya mazoezi ili kuepuka na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo hivi sasa unaongezeka kwa kasi na kupelekea vifo kwa jamii.

Mhe. Majaliwa aliendelea kusema kuwa ajenda ya mwaka 2030 ni kutomuacha mtu nyuma katika kupambana dhidi ya magonjwa ili kurahisisha utekelezaji azma ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Aidha,alisema jumuiya hiyo inatakiwa kuhimarisha ushirikiano hasa katika masuala ya Sekta ya Afya ili kuweza kusaidiana katika kutatua changamoto zinazoikumba Sekta hiyo baina ya mataifa hayo.



Monday, March 19, 2018

ALIYEKUWA RAIS WA AFRIKA KUSINI, JACOB ZUMA KUSHTAKIWA KWA MAKOSSA 16

Na Mwandishi Wetu
Immamatukio Blog

Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka 16. Mkurugenzi wa Mashtaka, Shaun Abrahams ameeleza kuwa Zuma atashtakiwa kwa makossa yakiwemo rushwa, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha.

Zuma anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na fedha za serikali na kusababisha hasara ya dola bilioni 2.5 kununulia silaha mwaka 1999, wakati huo Zuma akiwa ni Makamu wa Rais. Zuma alichaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini mwaka 2009 na kujiuzulu mwaka 2018 Februari akiwa amebakiza mwaka mmoja kabla ya kumaliza kipindi chake.

Zuma mwenye miaka 75, alijiuzulu Urais mwezi uliopita baada ya kulazimishwa na chama chake, African National Congress (ANC).







ZIMBABWE KUFANYA UCHAGUZI MWEZI WA SABA, 2018

Na Mwandishi Wetu
Immamatukio Blog.

Rais Emmerson Mnangagwa (pichani) wa Zimbabwe ametangaza jumamosi kuwa uchaguzi wa kwanza nchini humo wa Rais na Wabunge tangu kuondolewa madarakani Rais aliyeitawala Zimbabwe muda mrefu Robert Mugabe utafanyika mwezi julai.

Uchaguzi huo utakuwa ni jaribio la uongozi mpya uliotwaa madaraka mwaka jana novemba baada ya jeshi kulazimisha kujiuzulu kwa Mugabe (94). Pia itakuwa ni mara ya kwanza kufanyika uchaguzi bila sura ya Mugabe katika karatasi za kupigia kura toka mwaka 1980, ambapo nchi hiyo ilipopata uhuru toka kwa Mwingereza.

“Kama taifa, chama na serkali tunatarajia uchaguzi wa amani, uwazi na utulivu mwezi julai mwaka huu” alisema Mnangagwa mbele ya vyombo vya habari baada ya kukutana na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa jumamosi usiku.