
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave akizungumza na Wajumbe Wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Kigamboni, alipofanya ziara ya Kikazi katika Wilaya hiyo na Temeke, leo. Dorothy ambaye alifuatana na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT mkoa huo, amesisitiza kuwa ni lazima viongozi watambue kuwa muda wa maandalizi ya ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao ni sasa.

Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga akizungumza wakati wa kikao cha Kazi kati ya Mwenyekiti wa UWT mkoa huo na Wajumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT Wilaya ya Kigamboni, leo. Malyaga amesema UWT mkoa wa Dar es Salaam, Wanampongeza Rais Dk. John Magufuli kwa uthubutu aliofanya mwishoni mwa wiki iliyopita, kukutana na kufanya mazungumzo ya kina na Wafanyabiashara mbalimbali hapa nchini. "Sisi tunaaamini hatua hii itasaidia sana kuondoa au kupunguza changamoto zinazonyemelea sekta ya biashara nchini", alisema Tatu Malyaga

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave akiongozana na Wabumbe wa Baraza la Utekelezaji la mkoa huo, kuingia ukumbini wakati wa kikao hicho cha kazi Kigamboni. Kulia ni Wajumbe hao, Elizabeth Lameck na Hawa Nguh'umbi.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kigamboni Agnes Seng'unda akimwongoza Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga kwenda ukumbini. Kulia ni Katibu wa UWT Kigamboni Nasma Abdallah

Katibu wa CCM Wilaya ya Kigamboni Agnes Seng'unda akizungumza mwanzoni mwa kikao hicho cha kazi.

Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la UWT mkoa wa dar es Salaam, Elizabeth Lameck akisalimia baada ya kutambulishwa na Malyaga.

Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT mkoa wa Dar es Salaam Hawa Nguh'umbi akisalimia baada ya kutambulishwa.

Washiriki wa kikao hicho cha kazi wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave, Katibu wa UWT mkoa huo Tatu Malyaga na Wajumbe wa Baraza la Utekelezaji la UWT mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho cha kazi

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave akipewa chakula na mhudumu, wakati wa chakula cha mchana baada ya kikao hicho cha kazi

Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Tatu Malyaga akipewa chakula na mhudumu, wakati wa chakula cha mchana baada ya kikao hicho cha kazi

Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT mkoa wa Dar es Salaam, Elizabeth Lameck akipewa chakula na mhudumu, wakati wa chakula cha mchana baada ya kikao hicho cha kazi

Baadhi ya viongozi na washiriki wa kikao hicho cha kazi wakipata chakula. Kulia ni Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT mkoa wa Dar es Salaam Hawa Ngh'umbi.

Baadhi ya viongozi na washiriki wa kikao hicho cha kazi wakiwa kwenye foleni ya chakula.

Baadhi ya viongozi wa UWT Wilaya ya Kigamboni wakipata chakula.
TEMEKE

Ujumbe kutoka UWT mkoa wa Dar es Salaam wakipokewa na wenyeji kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Mtoni, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave na ujumbe wake huo walipowasili tayari kwa kikao cha kazi na viongozi wa UWT wa Wilaya ya Temeke.

Ujumbe ukiingia ukumibi

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave akisaini kitabu cha wageni

Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga akisaini kitabu cha wageni

Hawa Ngh'umbi akisaini kitabu cha wageni

Elizabeth Lameck akisaini kitabu cha wageni

Baadhi ya wajumbe wakienda ukumbini

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave (wapili kulia) akiwasili ukumbini na viongozi wenzake wa meza kuu. Kushoto ni Mjumbe wa baraza la Utekelezaji UWT mkoa wa Dar es Salaam Elizabeth Lameck, Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Tatu Malyaga na kulia ni Mwenyekiti wa UWT Kigamboni Rukia Kamal

Wajumbe wakishangilia ukumbini

Diwani wa viti Maalum Kassidi Likacha akisalimia baada ya kutambulishwa

Diwani wa viti maalum Mwanakombo Mwinyimbegu kisalimia baada ya kutambulishwa ukumbini

Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam tatu Malyaga akisalimia na kutoa utambulisho

Hawa Ngh'umbi akisalimia bada ya kutambulishwa

Wajumbe wakishangilia

Katibu wa UWT Kigamboni Kimenta Mavala akikabidhi risala kwa mgeni rasmi baada ya kuisoma

Mwenyekiti wa UWT Kigamboni Rukia kamal akifungua kikao

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave (kulia na Katibu wake Tatu Malyaga wakishangilia baada ya kikao kufunguliwa. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT mkoa wa Dar es Salaam Elizabeth Lameck

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave akisalimia kabla ya kuanza kuzungumza na wajumbe kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave akizungumza na wajumbe kwenye kikao hicho.

Wajumbe kwenye kikao hicho

Mjumbe akitoa hoja

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave akizungumza na wajumbe katika kikao hicho cha kazi kilichofanyika Temeke, Dar es Salaam leo

Katibu wa UWT Wilaya ya Kigamboni Kimenta Mavala akionyesha tuzo, kabla ya kukabidhiwa kwa Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave kwa kushika nafasi hiyo

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Rukia Kamal akikabidhi tuzo hiyo kwa Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave

Dorothy Kilave akionyesha tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa

Dorothy Kilave akionyesha tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT mkoa wa Dar es Salaam Elizabeth Lameck na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Tatu Malyaga

Tuzo hiyo

Diwani wa Viti Maalum CCM Mwanakombo Mwinyimbegu akimpongeza Dorothy Kilave

Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT Wilaya ya Temeke Nuru Kassian (kushoto) akiwa na Diwani wa Viti Maalum CCM Mwanakombo Mwinyimbegu mwishoni mwishoni mwa kikao hicho. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog
No comments:
Post a Comment