Monday, May 23, 2016

SWALI LILOMTUMBUA KITWANGA BUNGENI LAJIBIWA

Swali lililopelekea kutumbuliwa kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga limejibiwa rasmi na Naibu Waziri wa

Wakati akijibu swali hilo leo Bungeni,mjini Dodoma Mhandisi Masauni amefafanua kuwa katika kukabiliana na tatizo hilo serikali imeendelea na mpango wa kuzifanyia ukarabati mkubwa baadhi ya nyumba kwenye baadhi ya magereza na kujenga nyumba mpya.

Amesema mahitaji ya nyumba kwa sasa ni 14,500 wakati zilizopo ni 4,221 hivyo kuwepo kwa upungufu wa nyumba 10,279 ambao unalazimisha baadhi ya askari kuishi nje ya kambi za jeshi la magereza.

Aidha serikali kupitia jeshi la magereza limesaini mkataba na kampuni ya Poly Technologies ya China kwa kujenga nyumba 9,500 kwenye vituo vyote vya magereza nchini.

“Mgawanyo wa ujenzi wa nyumba hizo ni makao makuu ya magereza nyumba 472, Arusha 377, Dar es Salaam 952, Dodoma 356, Kagera 364, Kigoma 272, Kilimanjaro 390, Lindi 233, Manyara 206, Mara 378, Mbeya 622, Iringa 336, Morogoro 669, Mtwara 215 na Mwanza 398,".



"Pwani 384, Rukwa 358, Ruvuma 320, Shinyanga 337, Singida 299, Tabora 408, Tanga 382, KGKGM Dar es Salaam 219, Chuo cha Ukonga 115, Chuo cha kiwira 183, Chuo Ruanda 62, Chuo KPF 27, Bohari kuu 82 na Bwawani 84.”anasema.

Lakini pia amesema kwa upande wa jeshi la polisi,serikali inakusudia kujenga nyumba 4,136 katika mikoa 17 ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Anaongeza kuwa serikali itendelea kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba nafuu, miradi shirikishi PPP na kwa kutumia fedha za bajeti ya serikali kadri hali ya uchumi itakavyokuwa inaimarika.

"Mkakati huo utakwenda sambamba na mipango ya maendeleo ya serikali ikilenga kufikia idadi ya nyumba za makazi kwa askari wote waliopo sasa na watakao ajiriwa baadae".

Kwa upande wa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasinim katika swali la nyongeza alihoji kuwa suala la magereza limekuwa ni changamoto ya muda mrefu ambayo imekuwa ikizungumzwa kila kukicha lakini serikali haijafanya kazi ambapo alitaka ufafanuzi ni lini litafanyiwa kazi hususani kwenye jimbo lake ambalo askari wanaishi kwenye nyumba za mabanzi.

Mhandisi Masauni akijibu swali hilo anasemakwamba jeshi limeandaa andiko linaloainisha miradi nane ambalo limeshawakilishwa serikalini kwa ajili ya kufanyiwa kazi na kumuahidi kuwa ataungana nae kwenda kwenye Jimbo hilo la Rombo kujionea hali halisi mbali na kuwepo mchakato ambao unaendelea ambao ni wa kujenga nyumba 38.  
                               
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akizungumka katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari.


No comments:

Post a Comment