Monday, June 11, 2018

KITUO CHA AFYA TAMOTA - BUMBULI VIJIJI 20 KUNUFAIKA


PICHANI: Moja ya majengo ya Kituo cha Afya Tamota, Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo January Makamba alikagua ujenzi wake jana Juni 10, 2018. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).

Na Yusuph Mussa, 
Immamatukio Blog, 
Lushoto

WANANCHI wa vijiji zaidi ya 20 wanatarajiwa kunufaika na ujenzi wa Kituo cha Afya Tamota kilichopo Kijiji cha Tamota, Tarafa ya Bumbuli, Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Ni baada ya Serikali Kuu kutoa sh. milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa majengo muhimu kwa iliyokuwa Zahanati ya Tamota ili kuwa Kituo cha Afya.

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba jana Juni 10, 2018 alitembelea Kituo cha Afya Tamota kuona ujenzi unavyoendelea ambapo kwa sasa ujenzi wake umefikia hatua ya linta.

Baadhi ya majengo yanayojengwa ni wodi ya wanawake ikiwemo wazazi, maabara, upasuaji na nyumba ya mtumishi, ambapo hadi sasa ujenzi huo umegharimu sh. milioni 135.6

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Afisa Mtendaji wa Kata ya Tamota Sophia Matogolo alisema kati ya fedha hizo, wananchi wamechangia sh. milioni 10 ikiwa ni pamoja na kuchota maji na kuchimba msingi wa majengo hayo.

Katibu wa Mbunge ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kwamkomole, Hozza Mandia alisema kituo hicho kitamaliza matatizo ya wananchi kupata huduma za afya kwenye kata za Tamota, Mahezangulu na Funta katika Jimbo la Bumbuli.

"Pia kitatoa huduma kwa kata jirani za Wilaya ya Korogwe za Mpale, Dindira na Mgwashi. Na baadhi ya huduma zitakuwa zimeboreshwa sana kama upasuaji na mama kujifungua kwa uhakika.

"Huo ni ushindi mkubwa kwa wananchi wa vijiji zaidi ya 20 kwenye kata hizo kwa vile walianza kuomba kituo hicho zaidi ya miaka saba iliyopita, lakini Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli na Mbunge January Makamba ndiyo wamefanikiwa kupata Kituo cha Afya" alisema Mandia.

Ujenzi wa majengo hayo ambao ulikuwa ukamilike kwa miezi mitatu, ulisimama kutokana na mvua, hivyo unatarajiwa kukamilika baada ya mwezi mmoja, na hadi kukamilika kwake utagharimu sh. milioni 400.

Moja ya majengo ya Kituo cha Afya Tamota, Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo January Makamba alikagua ujenzi wake jana Juni 10, 2018. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio blog).



Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (mwenye kanzu) i alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa baadhi ya majengo mapya ya Kituo cha Afya Tamota jana Juni 10, 2018. Wa pili kulia ni Katibu wa Mbunge Hozza Mandia na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi huo Abdallah Shemavunde. (Picha na Yusuph Mussa,Immamatukio blog)

Viongozi wa Halmashauri ya CCM Kata ya Tamota muda mfupi kabla ya kuanza kikao na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (hayupo pichani) kwenye Kijiji cha Tamota. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio blog).


7 comments:

  1. Hawa ni wananchi au viongozi wa halmashauri ya Kata? Muandishi hii habari ulikuwepo au ulitumiwa??

    ReplyDelete
  2. Best fitness band in India. Track your workout and get the best fitness tracker under 2000. Hop and shop the best best fitness band Or fitness tracker india under 2000. The best fitness tracker under 2000. best fitness band under 2000 in india

    ReplyDelete
  3. Find and hire best top models, singers, influencers with good followers and celebrities managers for work. Hire freelance models, freelance singers, freelance male or female actress in India. jobs for modeling

    ReplyDelete
  4. Get yourself updated with the latest and trending web series going viral. One place for all your viral news, youtube videos etc. viral news in hindi

    ReplyDelete
  5. Checkout the best special good morning, inspirational quotes, stories, motivational suvichar, success, love, life thought in hindi. motivational quotes hindi

    ReplyDelete
  6. Buy the Best solo microwave oven in India, best convection microwave oven under 5000,
    10000, 15000. best microwave convection oven

    ReplyDelete