Ajali mbaya na ya kutisha imetokea leo alfajiri katikati ya madaraja mawili ya chuma yaliyoko eneo la Kawe pembeni ya kambi ya JKT Mlalakuwa, Dar es Salaam.
Ajali hiyo mbaya iliyotokea na kusababisha dereva kupoteza maisha na kuacha vipande vya ubongo vikinin'ginia(PICHA YA 9) katika moja ya madaraja hayo, ilitokea wakati derevea huyo akiwa kwenye mwendo mkali na kushindwa kulimudu gari hilo aina ya Toyota Celica GTR yenye namba za usajili T220ABL(PICHA YA 11) na kuingia kwenye ukingo wa daraja(PICHA 2) na kisha kutumbukia kwenye mto unaopeleka maji baharini.
Inadaiwa maiti iliondolewa asubuhi wakati ajali hiyo ilitokea kati ya saa 8 na saa 9 alfajiri.
Juu na Chini: Mabaki ya gari liliopata ajali likitolewa na break down (Haipo Pichani) leo asubuhi
ANGALIA PICHA ZAIDI...
Mmoja wa mashuhuda (alikataa kutaja jina lake) akitoa vipande vya nguo katika sehemu ya nyuma ya gari hilo kama alivyokutwa na mpiga picha wetu
Juu na Chini: Picha inayoonesha kipande cha nyama inayodaiwa kuwa ni sehemu ya ubongo wa dereva huyo kikiwa kinanin'ginia katika daraja hilo. chini ni sehemu ya kioo cha mbele kilicho haribiwa vibaya na kubaki na sehemu ya damu
Tujiulize tunapokuwa tunaendesha mwendo kasi wa nini tena mijini?Tuwe makini
ReplyDeletemmmmmhhh hii ni balaaa sana poleni wafiwa wote ila hamjatuambia dereva alikuwa anaitwa nani plsssss
ReplyDeleteanaitwa Max
ReplyDelete