Showing posts with label BEAUTY. Show all posts
Showing posts with label BEAUTY. Show all posts

Wednesday, May 24, 2017

RASTAMAN MZEE WA MIAKA 110, BADO ANA NGUVU NA ANAIMBA MSIKILIZE HAPA

Rasta mzee anayedaiwa kuwa na miaka 110, akiimba nyimbo 'By the rivers of Babylon' Msikilize hapa chini



Sunday, June 08, 2014

MSHINDI WA MISS MBAGALA APATIKANA


Mshindi wa wa kwanza wa mashindano ya Miss Mbagala Amina Salum (kushoto) akipokea zawadi ya seti ya dekoda ya Dstv kutoka kwa Meneja wa mashindao hayo Gervas Sinsakala, mashindano hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Dar Live mwishoni mwa wiki

Thursday, June 05, 2014

FLAVIAN MATATA AZIDI KUJICHANGANYA NA WATU MAARUFU DUNIANI

Flavian Matata(kushoto) akiwa na Russel Simons(mwanaume), katika usiku wa kuwapongeza Simons na Kimora kwa mchango wao uliosababisha kuleta mabadiliko ya watu wengi maishani.

Chini: Flavian Matata katikati akiwa na bunifu maarufu duniani, DKNY (Dona Karan, New York-Kushoto) na mpiga picha wa fashion RussellJames, mtu aliyefanya naye kazi kwa mara ya kwanza nchini Marekani - Hongera sana Flavian



Wednesday, June 04, 2014

WALIMBWENDE WANAOWANIA TAJI LA MISS UBUNGO

Hawa ndio warembo wa Miss Ubungo, kama wanavyoonekana wakiwa kambini kama walivyokutwa na kamera yetu.

Wednesday, May 28, 2014

HAPPINESS MAGESA KUFUNGUA HOSPITALI YA WANAWAKE NCHINI

Miss Tanzania 2010 Happiness Magesa ametangaza nia yake rasmi ya kutaka kupata hospitali ya wanawake tanzania ili kuweza kuwasaidia katika suala la matatizo ya uzazi. Happness alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwakua yeye kashasumbuliwa sana na tatizo la uzazi kitaalamu wanaita Endrometriosis.

Happness alisema kuwa htaki wakina dada na wakina mama kuweza kuendelea kuteseka kama alivyoteseka yeye kwa mika mingi na hadi kufikia sasa ameshafanyiwa upasuaji zaidi ya mara kuminambili huko South Afrika.

Alisema tatizo hilo ni baya sana kwa kina mama kwani husababisha kupoteza matumaini ya kupata mtoto kama ilivyo yeye lakini anashukuru kwa sasa amejikwamua kwa hilo ndio mana anahitaji kusaidia a wengine.

"Ukweli kama mtanzani ambaye nimeteseka kwa muda mrefu na tatizo la uzazi nilikua sipendi na wezangu wanaonizunguka kuweza kuteseka huku akijua kama kuna tiba mbadala,"alisema

Alisema yeye pamoja na kampuni ya Magesa Foundation itahakikisha wataomba kila sehemu ilikuweza kupata walau sehemu ndogo kwa ajili ya kufungua hospitali ya wanaake kwa ajili ya kuwasadia wanawake wote wanao sumbuliwa na tatizo hilo.

Sunday, May 11, 2014

DIAMOND AINGIZWA MJINI MCHANA KWEUPEEE...


Msanii wa musiki wa kizazi kipya Diamond Platnums (Pichani Juu)  amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzidiwa spidi na wajanja ambao walirelease nyimbo yake baada tu ya kurekodi na wakati bado haija kamilika.

nyimbo hiyo inayodaiwa itaitwa "Kitorondo" iliibwa na kutoka bila yeye mwenyewe kujua imetokaje. Ilimlazimu Diamond kutuma ujumbe na kuomba hadhara isutumie wimbo huo rasmi. Katika ujumbe wake alioandika jana tarehe 10/04/2014, Diamond aloomba wimbo huo ambao haujakamilika rasmi usitumike kwenye vyombo vya habari, au hadharani.


Thursday, May 08, 2014

FASHIONISTAS: MARIAH CAREY AVALISHWA NA ROBERTO CAVALLI,ANGALIA CATWALK YA DIOR

JUU: Stage ya maonesho ya ubunifu wa nguo za mbunifu maarufu duniani Dior katika "Dior Cruise 2015", fashion show ilifanyika jana, jijini New York, nchini Marekani

Chini ni kazi ya mbunifu Roberto Cavalli

Msanii mwimbaji wa music wa RnB Mariah Carey akiwa na watoto wake katika mavazi yaliyobuniwa na Roberto Cavalli. Chini ni maandalizi ya fashion show ya Dior Cruise 2015, katika back stage, chini kabisa ni onesho la Dior Cruise 2015 likiwa linaendelea.



Wednesday, May 07, 2014

HAWA NDIO WAREMBO WA REDS MISS DAR CITY CENTER

 Warembo wakiwa wamejipanga jukwaani katika uzinduzi wa mchakato wa kumtafuta mlimbwende wa Reds Miss Dar City Center jumamosi iliyopita katika ukumbi wa Escape1



Thursday, April 24, 2014

FASHIONISTA: LUPITA AZIDI KUNG'ARA, ANGALIA MITINDO MIPYA HUMU

 Juu: Sura ya gazeti toleo jipya la People, Lupita Nyong'o ang'ara katika wanawake 50 warembo zaidi
Chini : Toleo jipya la stileto hill, la Roberto Cavalli


Tuesday, April 08, 2014

FASHIONISTAS; ELEGANT DESIGN BY ROBERTO CAVALLI

An extreme attention to details and finish are the most important part of the RobertoCavalli collections




Wednesday, March 12, 2014

LUPITA NYONG'O NA FASHION, UKIANZA KUTOKA UNATOKA TU


LUPITA NYING'O ilikuwa ni suala la muda tu, cheki hapa kaukwa na u-model, hapa anatangaza kampeni mpya ya MiuMiu SS2014 ambayo ni mikoba ya wanawake.

Wednesday, March 05, 2014

FASHIONISTAS: NYOKA WANAVYOGEUZWA KUWA MIKOBA ILI UPENDEZE

Je unatumia bidhaa kama mikanda, mabegi, viatu na wakati mwingine nguo zinazotumia ngozi ya nyoka, leo nakuletea picha hapa uone jinsi nyoka wanavyouawa na kuchunwa ngozi ili wewe upendeze.

Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuua na kuchuna ngozi ya nyoka huko Indonesia. Lakini njia ambayo ni ukatili ambapo nyoka wanauawa na kuchunwa ngozi kwaajili ya kutengeneza mikoba haswa na kuuzwa nchi za Magharibi kwa zaidi ya shilingi milioni 6.5 (pauni za Uingereza 2400).

Pamoja na gharama yote hiyo huko Ulaya na Marekani, mkoba huo unapatikana kwa sawa na shilingi za Kitanzania 54,000(pauni 20) nchini Indonesia kwenye soko la ngozi ya nyoka ambapo nguo na vipuri mbalimbali huuzwa.

Moja ya machinjio ya nyoka yalionesha jinsi nyoka wanavyovuliwa ngozi yao ni kijiji kimoja kijulikanacho kama Cirebon, nchini Indonesia. Ukiangalia katika picha hizi utaona jinsi wafanyakazi wanavyoua na kuchuna ngozi nyoka zaidi ya elfu kwa wiki.

Katika maeneo hayo bei ya mkoba uliotengenezwa kwa ngozi ya nyoka unaweza kuwa kati ya shilingi 24,000(pauni9) mpaka 48,000 kutegemea na ukubwa. Ngozi ya nyoka inapofika nchi za Magharibi katika nyumba za mitindo bei hupanda maradufu mpaka awa na shilingi milioni 6.5

ANGALIA ZAIDI...