Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa ofa maalum kwa Mwanamuziki, Ally Kiba, mke wake na wasaidizi wake ambao ni mdogo wake Abdu Kiba na mkewe kupumzika katika Hifadhi ya Taifa atakayoichagua wakati wa fungate yake ili aweze kufurahi vivutio vya utalii vilivyopo na hivyo kuhamasisha utalii wa ndani. Ametoa ofa hiyo jana wakati wa harusi ya msanii huyo iliyofanyika katika ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa sherehe hiyo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde na Mbunge wa Viti Maalum, Neema Mgaya.














