Kulia ni Mwenyekiti wa mashindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 na kushoto ni katibu wa kamati ya mshindano hayo walipokuwa wakiongea na vyombo vya habari kwenye ofisi zao zilizopo manispaa ya Iringa mkoani Iringa mapema hii leo
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Kamati ya ya mshindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 imezindua rasmi kwa kuanza kuzialika timu kwa ajiri ya kuchukua fomu kushiriki na wameweka bayana jinsi mfumo wa mashindano utakavyokuwa pamoja na zawadi kwa washindi wote.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa mashindano hayo Gerald Malekela alisema kuwa analialika timu mbalimbali za mkoa wa Iringa kuja kuchukua fomu za mashindano kwa gharama ya shilingi elfu thelathini (30,000/=) ambazo zinapatikana katika kituo cha radio cha Nuru Fm.
“Naomba viongozi wa vilabu vinavyotaka kushiriki mashindano haya vinatakuwa kufika katika ofisi za Nuru fm au kumpigia mratibu wa mashindano haya Fredy Mgunda kwa kumpigia simu ya nambari 0714201006 au mnipigie mimi mwenyewe kwa namba hii 0762687732 hapo utakuwa umerahisisha jinsi ya kuzipata hizo fomu na maelezo kwa kina” alisema Malekela

















