Wednesday, November 25, 2015

BINTI ALIYEJIUNGA ISIS APIGWA MPAKA KUFA ALIPOJARIBU KUTOROKA

Samra Kesinovic, 17, pichani kushoto aliondoka Austria mnamo 2014 mwezi aprili akiwa na rafiki yake Sabrina Selimovic, imedaiwa amepigwa na magaidi wa kundi la magaidi wa Kiislam wa ISIS mpaka kupoteza maisha wakati alipojaribu kutoroka eneo la Raqqa.

Inaaminika kuwa Sabina alifariki mwezi disemba mwaka jana wakati wa kipindi cha mapigano makali. Wasichana hao wawili walionekana katika video ya propaganda za ISIS mda mfupi baada ya kuwasili nchini Syria. Rafiki yake ambaye waliambatana aliuwawa miezi michache kabla yake.

Samra Kesinovic na rafiki yake Sabina Selimovic(kulia) wakiwa katika picha iliyopigwa na kundi la magaidi wa ISIS mda mfupi baada ya kuwasili nchini Syria mwezi aprili 2014.


FAMILIA YA MTOTO ALIYESINGIZIWA KUBEBA BOMU YADAI BILIONI 32

Familia ya mtoto wa Kiislamu aliyekamatwa baada ya kubuni na kutengeneza saa yake na kuipeleka shuleni kisha kudahiniwa kuwa amebeba bomu, wanadai fidia ya dola milioni 15(sawa na takribani shilingi bilioni 32 za Kitanzania)

Familia ya Ahmed Mohamed pia wanadai kuombwa radhi na jiji la Irving pamoja na shule baada ya kijana huyo wa miaka 14 kukamatwa na polisi mwezi wa tisa mwaka huu.

Kwa mujibu wa gazeti la NY Daily, mwanasheria anayewakilisha familia hiyo alituma barua katika jiji la Irving, lililoko mashariki mwa Dallas pamoja na shule ya Wilaya ya Irving Independent School nchini Marekani, akielezea kuwa mwanafunzi huyo wa darasa la tisa alisingiziwa na kukamatwa kisha kuwekwa rumande na kuhojiwa bila wazazi uwepo wa wake.

Familia ya Mohamed inalidai jiji dola za Marekani milioni 10 (sawa na takribani shilingi za Tanzania bilioni 21) pamoja na shule ya wilaya hiyo dola milioni 5(sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 11) lasivyo watafungua kesi ndani siku 60, barua hiyo ilieleza.

BOFYA KUONA KAZI YA MTOTO HUYO. . .


MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI KUFANYIKA SINGIDA


Maambukizi ya ukimwi yameongezeka kwenye kundi la vijana wenye umri wa miaka kati ya 19 mpaka 24 tofauti na ilivyokuwa miaka minne iliyopita, ambako kundi lililokuwa limeathiriwa zaidi lilikuwa miaka kati ya 25 mpaka 34, imeelezwa pia licha ya kwamba kiwango cha maambukizi mapya ya virusi hivyo nchini kimeshuka kutoka asilimia 7 mwaka 2004 mpaka kufikia asilimia 5.3 mwaka huu, takwimu za baadhi ya mikoa ikiwemo Singida, Kigoma,Arusha, Mtwara, Kilimanjaro na Kagera zimeonekana kuongezeka.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani kwa mwaka huu, Dk.Fatma Mrisho(pichani juu), alisema kazi kwa ujumla kazi kubwa imefanyika.


Tuesday, November 24, 2015

MAKAMU WA RAIS ATETA NA MTANDAO WA WANAWAKE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na uongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania (WFT) ambapo amezungumzia dhamira ya serikali katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo mbali mbali yanayowakabili wanawake na watoto wa kike nchini.

Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais aliueleza ujumbe huo kuwa wakati wa kampeni aliahidi pamoja na kazi za kumsaidia Mhe. Rais bado kama mama atafuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi ya kupatikana kwa maji safi na salama, kuboresha afya ya mama na mtoto, elimu na mazingira.

“Nilipokuwa kwenye kampeni nimejionea shida ya maji na wanawake ndiyo wanaopata tabu ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji. Kwa hiyo, pamoja na kazi zangu za kumsaidia Mhe. Rais nitasimamia miradi yote ya maji, alau tuhakikishe maji yanapatikana umbali wa mita 400 kutoka eneo wananchi wanakoishi au karibu zaidi”.


RC KILIMANJARO AKUTANA NA MAOFISA WA MANISPAA KUJADILI HOFU YA KIPINDUPINDUMkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akiwa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,kuzingumza na watendaji wa Afya na Mazingira.

MBUNGE WA CHUMBUNI APOKELEA NA WAPIKA KURA KWA SHANGWE AKITOKEA DODOMA
Mhe Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akipongezwa na Mke wakati alipofika kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa wiki iliopita.

Monday, November 23, 2015

BREAKING NEWS:SHEREHE ZA UHURU KUTOFANYIKA MWAKA HUU“Rais Dr. John Pombe Magufuli ameamuru kuwa siku ya Uhuru yaani 9 December hakutakuwa na shamra shamra zozote watu wote watafanya usafi wa mazingira ili kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kwa maana hiyo hakutakuwa na sherehe za magwaride katika uwanja wa Uhuru kama ilivyozoeleka” amesema Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo

BIMA YA AFYA NHIF YAKANUSHA KUDAIWA NA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA


Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini umekanusha kuwepo kwa madai yaliyotolewa na Hospital ya Rufaa Mkoani Mbeya kuwa wanaudai Mfuko jumla ya shilingi bilioni 2 na kwamba wanaudai Mfuko kutoka mwezi Juni, 2015.

Akizungumza jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Ndugu Michael Mhando amesema madai yaliyotolewa na Hospital hiyo ya Rufaa Mkoa wa Mbeya hayana ukweli wowote nakwamba mfuko huo unalipa madai baada ya mtoa huduma kuwasilisha kwenye Mfuko.

STANDARD CHARTERED BANK YAPATA MKURUGENZI WA KWANZA MTANZANIA

SANJAY RUGANI  
MKURUGENZI MKUU
STANDARD CHARTERED BANK TANZANIA WAKENYA WAJIANDAA KUMPOKEA PAPA FRANCIS, ULINZI KUIMARISHWA

Serikali ya Kenya imesema maandalizi ya kumlaki Papa Francis nchini Kenya yamekamilika na ziara yake inatarajiwa kuwa ya kufana.

Kwenye kikao na wanahabari, Msemaji wa Ikulu Manoah Esipisu na Inspekta Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet walisema hatua madhubuti zimechukuliwa kumpokea kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani.

“Hili ni tukio muhimu sana, nchi yetu inamkaribisha Papa Francis kwa mara ya kwanza barani Afrika, na ningependa kusema kwamba tuko tayari kumpokea pamoja na msafara wake, usalama umeimarishwa tukiangazia kuanzia kuasili kwake, njia atakazotumia na pia kwa wageni wote watakaomiminika jijini hapa,” alisema Bw Boinnet.

JAMAA ALIYEBADILI JINSIA AJIUA, KISA KAHUKUMIWA KWENDA JELA YA WANAUME

Mwanaume aliyebadili jinsia na kuwa mwanamke aliyetishia kujiua iwapo angepelekwa jela ya wanaume, amekutwa amekufa. Vicky Thompson (PICHANI KULIA), mwenye umbra wa miaka 21, alihukumiwa kifungo cha miezi 12 katika jela ya HMP Leeds baada ya kuvunja makubaliano ya hukumu aliyopewa awali.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror la niching Uingereza, Mwanasheria wa Vicky, Mohammed Hussain alimweleza hakimu kuwa Vicky ni mwanamke na kumtaka ampeleke kutumikia kifungo chake katika mahakama ya New Hall kitengo cha wanawake, karibu na Wakefield.


ARUSHA SASA KUFURAHIA INTANETI YA KASI ZAIDI KUTOKA TIGO

Arusha, Novemba 18 2015. Wateja wa Tigo waishio Arusha sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.

‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es Salaam kuanzia mapema mwaka huu’’, amesema Mkuu wa Kitengo cha Internet David Zacharia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Zacharia amesema: "ni kielelezo cha jinsi ambavyo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya dijitali katika maisha ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia teknolojia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania."


MILEY CYRUS KAZIDISHA. . ., AMNYONYA DANCER WAKE MATITI JUKWAANI (ANGALIA PICHA)Tunajua kichaa chake, usiku wa alhamisi iliyopita, Miley Cyrus (KUSHOTO PICHANI) alifanya kituko ambacho hakijawahi kutokea akiwa jukwaani, wakati akifanya onesho la kukata na shoka jijini Chicago.

Aliingia jukwaani katika ukumbi wa Rivera akiwa amevalia vazi la aibu mno ambalo linaonesha maungo yake na uume wa bandia. 

Lakini kama haitoshi alimnyonya mcheza sho wake maziwa akiwa jukwaani. . . 

Bofya uangalie picha chini. . .


KANDA YA KASKAZINI WAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIAMwenyekiti wa kamati ya maandalizi uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini na Meneja Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la NAFGEM,Honorata Nasuwa akizungumza na wanahabari(hawako pichani ) juu ya uzinduzi huo,kushoto kwake ni Afisa Ushawishi na utetezi (KWIECO) na mratibu wa maadhimisho hayo kanda,Hilary Tesha.

Sunday, November 22, 2015

PANONE FC YASONGA MBELE LIGI YA SHIRIKISHO YA AZAM,YAIFUNGA POLISI 2 - 1.


Wachezaji wa timu ya soka ya Panone fc wakipasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mchezo wa ligi ya shirikisho inayodhaminiwana Azam.