Sunday, June 03, 2018

MAPACHA WALIOUNGANA CONSOLATA NA MARIA WAFARIKI DUNIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.


Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na kifo cha mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia jana jioni katika hospitali ya Mkoa wa Iringa.

Mhe. Rais Magufuliwa aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam tarehe 06 Januari, 2018.

Pamoja na kuwapa pole Maria na Consolata waliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake.

Mhe. Rais Magufuli anasema anatambua kuwa Maria na Consolata walikuwa na ndoto kubwa ya kuja kulitumikia Taifa baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Masista wa Consolata Ruaha (RUCO) walikokuwa wakiendelea na masomo yao, lakini haikuwa hivyo.

Maria na Consolata walikuwa watoto yatima, na walikuwa wakilelewa na kusomeshwa na Masista wa Maria Consolata wa Kanisa Katoliki. Amewaombea Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi, Amina. 









Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali pamoja na watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.


1 comment:

  1. KARAT - online casino | KADangPintar
    Welcome to KARAT. Welcome to KARAT Casino. Our brand is built for fun, play and gaming. Register today and start 온카지노 가입쿠폰 playing today!

    ReplyDelete