PICHANI: Moja ya majengo ya Kituo cha Afya Tamota, Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo January Makamba alikagua ujenzi wake jana Juni 10, 2018. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).
Na Yusuph Mussa,
Immamatukio Blog,
Lushoto
WANANCHI wa vijiji zaidi ya 20 wanatarajiwa kunufaika na ujenzi wa Kituo cha Afya Tamota kilichopo Kijiji cha Tamota, Tarafa ya Bumbuli, Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
Ni baada ya Serikali Kuu kutoa sh. milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa majengo muhimu kwa iliyokuwa Zahanati ya Tamota ili kuwa Kituo cha Afya.
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba jana Juni 10, 2018 alitembelea Kituo cha Afya Tamota kuona ujenzi unavyoendelea ambapo kwa sasa ujenzi wake umefikia hatua ya linta.
Baadhi ya majengo yanayojengwa ni wodi ya wanawake ikiwemo wazazi, maabara, upasuaji na nyumba ya mtumishi, ambapo hadi sasa ujenzi huo umegharimu sh. milioni 135.6
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Afisa Mtendaji wa Kata ya Tamota Sophia Matogolo alisema kati ya fedha hizo, wananchi wamechangia sh. milioni 10 ikiwa ni pamoja na kuchota maji na kuchimba msingi wa majengo hayo.
Katibu wa Mbunge ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kwamkomole, Hozza Mandia alisema kituo hicho kitamaliza matatizo ya wananchi kupata huduma za afya kwenye kata za Tamota, Mahezangulu na Funta katika Jimbo la Bumbuli.