Saturday, April 12, 2014

MVUA INAVYOTISHIA AMANI DAR ES SALAAM, ANGALIA MAFURIKO HAYA

 Nyumba zilizoko eneo la Jangwani, Manispaa ya Ilala pembezoni mwa barabara ya Morogoro, zikiwa zimezama katika maji yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salam na nchi nzima. baadhi ya nyumba kama zinavyoonekana bado umeme unawaka, kitu ambacho ni hatari kwa maisha ya watu.
Chini ni eneo la Jangwani barabara ya Morogoro, imekuwa shida kwa magari kupita kama inavyoonekana katika picha hali ambayo inaendelea mpaka sasa hivi.

 Chini: Kijiko cha kampuni ya kutengeneza barabara ya Strabag kikiwa kimezama kwenye maji wakati kikiwa kimebeba baadhi ya maofisa wa kampuni hiyo kuwaondoa katika eneo lilizungukwa na maji, pembezoni mwa barabara ya Morogoro kama picha inavyoonesha.



 Wakazi wa eneo la Jangwani wakiokota chupa chakavu kwenye maji kama wanavyoonekana pichani.

 Wakazi wa mabondeni ambao nyumba zao zimefunikwa na maji wakiwa wamejisitiri katika kituo cha mabasi ya mwendo kasi ambacho hakijaisha katika eneo la Jangwani, barabara ya Morogoro kama walivyokutwa na mpiga picha wetu dakika chache kabla ya kwenda mtamboni.

Juu ni barabara ya Umoja wa Mataifa karibu na shule ya sekondari ya Tambaza, jijini Dar es Salaam, maji yamefurika na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.
Chini ni gari la kampuni ya kutengeneza barabara ya mabasi ya mwendo kasi eneo la Jangwani likiwa limenasa na kuzama katka maji kama linavyoonekana.



5 comments:

  1. hivi hawa engeers wenye degree waliojazana Tanzania hawana uwezo wa kudizain mfumo wa kutoa maji ya mvua mjini? au ndo makanjanja?

    ReplyDelete
  2. Yaani hata haieleweki maana wengine ndio kama unavyowaona kwenye picha hapo juu wanafanya kubebwa na kijiko kutolewa, sijui tumefika wapi kwa kweli?!

    ReplyDelete
  3. To sum it up, Huu mji haukupangwa kuzingatia tabia za mvua na historia ya mafuriko toka mkoloni aachie madaraka. mji umevurugwa, watu wamwvurugwa sasa mwenye mach haambiwi tazama na kila mtu akili kichwani mwake.

    ReplyDelete
  4. Agree, imefikia wakati sasa watanzania tubadilike maana ni kama tunaendeshwa tukiwa tumelala hakuna aliye serious na kitu chochote, ni mafundi wa kulalamika na maneno mengi lakini vitendo sifuri

    ReplyDelete
  5. da poleni enyi wkazi wa jangwani lakini next time mfuate ushauri wa serikali wa nyie kuhama najua maisha ni magum may mnaweza mkawa na vitu ambavyo mkihama kuvipata itawkost but maisha ni boro kuliko kitu chochote

    ReplyDelete