Sunday, May 11, 2014
DIAMOND AINGIZWA MJINI MCHANA KWEUPEEE...
Msanii wa musiki wa kizazi kipya Diamond Platnums (Pichani Juu) amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzidiwa spidi na wajanja ambao walirelease nyimbo yake baada tu ya kurekodi na wakati bado haija kamilika.
nyimbo hiyo inayodaiwa itaitwa "Kitorondo" iliibwa na kutoka bila yeye mwenyewe kujua imetokaje. Ilimlazimu Diamond kutuma ujumbe na kuomba hadhara isutumie wimbo huo rasmi. Katika ujumbe wake alioandika jana tarehe 10/04/2014, Diamond aloomba wimbo huo ambao haujakamilika rasmi usitumike kwenye vyombo vya habari, au hadharani.
Kwa mujibu wa taarifa yake aliyoweka katika mtandao wa Instagram, Diamond aliandika "Moja ya nyimbo zangu ambazo ziko store hazijatoka nimeikuta mtandaoni na sijui imefikaje, tena ikiwa kwenye mfumo wa Voicenote."
Diamond ambaye ni msanii aliejipatia umaarufu mkubwa hivi karibu aliibuka kidedea kwa kunyakua tuzo saba mfululizo za Kilimanjaro Music Award 2014, ambazo hufanyika kila mwaka, ikiwa ni rekodi ambayo haijawahi kutokea toka kuanza tuzo hizo.
Diamond alilalamika kwamba nyimbo hiyo ambayo hakuitaja jina lake ambayo mtandao wa Imma Matukio iliweza kuhusikia wanamtandao wajamii wamedai unaitwa "Kitororo" na kudhibitisha kuwa ni kweli haina kiwango cha kuingia mtaani rasmi.
"Yaani haina quality kabisaa… Tafadhari, kwa yeyote atakayeipata asiitumie kwenye media ama hadharani, kwasababu haijatoka na haiko qualified…" alimaliza Diamond.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment