Wednesday, May 28, 2014

HAPPINESS MAGESA KUFUNGUA HOSPITALI YA WANAWAKE NCHINI

Miss Tanzania 2010 Happiness Magesa ametangaza nia yake rasmi ya kutaka kupata hospitali ya wanawake tanzania ili kuweza kuwasaidia katika suala la matatizo ya uzazi. Happness alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwakua yeye kashasumbuliwa sana na tatizo la uzazi kitaalamu wanaita Endrometriosis.

Happness alisema kuwa htaki wakina dada na wakina mama kuweza kuendelea kuteseka kama alivyoteseka yeye kwa mika mingi na hadi kufikia sasa ameshafanyiwa upasuaji zaidi ya mara kuminambili huko South Afrika.

Alisema tatizo hilo ni baya sana kwa kina mama kwani husababisha kupoteza matumaini ya kupata mtoto kama ilivyo yeye lakini anashukuru kwa sasa amejikwamua kwa hilo ndio mana anahitaji kusaidia a wengine.

"Ukweli kama mtanzani ambaye nimeteseka kwa muda mrefu na tatizo la uzazi nilikua sipendi na wezangu wanaonizunguka kuweza kuteseka huku akijua kama kuna tiba mbadala,"alisema

Alisema yeye pamoja na kampuni ya Magesa Foundation itahakikisha wataomba kila sehemu ilikuweza kupata walau sehemu ndogo kwa ajili ya kufungua hospitali ya wanaake kwa ajili ya kuwasadia wanawake wote wanao sumbuliwa na tatizo hilo.

Pia aliwaomba wasanii kama vile Wema sepetu, Lulu na lina kuweza kufikisha ujumbe kwa watanzania kwamba endapo watakuwa wanasikia maumivu chini ya tumbo basi wawahi hospitali kwa ajili ya kupata tiba ya haraka.


No comments:

Post a Comment