Dada anavituko, acha tu…kama umekuwa unamfuatilia Nicki Minaj katika mitandao ya kijamii, wiki hii alikuwa na ugomvi na Farrah Abraham, huku pamoja na hilo akiwa akijikumbusha mambo kadhaa wakadha ya mwaka 2013 katika gazeti la Elle.
Staa huyo wa “Anaconda” amekuwa akiweka picha zake za zamani huku akiongea na mashabiki kuhusu vituko vyake katika video yake ambapo alicheza kama mwandishi wa gazeti la Elle akiitwa Nicole, alijihoji maswali yeye mwenyewe.
Jumanne (12Januari) aliwaambia mashabiki wake kwa kupitia mtandao wa Twitter kuwa wafungue video hiyo ya mwaka 2013. Na ukiangalia mahojiano hayo ambayo kwa kweli ni mazuri ukiacha tu kwamba yalizungumzia zaidi enzi za utotoni wake.
No comments:
Post a Comment