Microsoft imetangaza kwamba imeacha kutoa usaidizi wa kiufundi kwa matoleo ya awali ya kisakuzi chake cha Internet Explorer na kuwaweka hatarini mamilioni ya watu wanaotumia matoleo hayo.
Mabadiliko hayo yataathiri matoleo nambari 8, 9 na 10 ya kisakuzi hicho.
Ukosefu wa usaidizi wa kiufundi na maboresho huweka watu mitambo inayotumia visakuzi hatarini ya kuvamiwa na wadukuzi na kuambukizwa mitaliga ama virusi.
Baadhi ya mashirika yanakadiria kwamba matoleo hayo hutumiwa na takribani asilimia 20 ya Computerworld inasema kati ya watu wanaotumia Internet Explorer, ni asilimia 55 pekee wanatumia matoleo ya majuzi zaidi.
Visakuzi hulengwa na wadukuzi na wataalamu hubashiri uwezekano wa mashambulio kutokea na kuweka kinga kupitia kutoa matoleo mapya. "Kuanzia Januari 12, 2016, ni toleo la karibuni zaidi la Internet Explorer litapokea usaidizi wa kiufundi na maboresho ya kiusalama,” Microsoft wamesema.
"Microsoft inawahimiza wateja kuboresha na kutumia toleo la majuzi zaidi na ili kuchakura mtandaoni kwa njia salama zaidi.” Kampuni hiyo inaendelea kutoa usaidizi kwa matoleo ya IE 11 na Edge, ambayo kimsingi ndiyo hutumiwa na Windows 10.
NetMarketShare inakadiria kwamba wanaotumia Internet Explorer mtandaoni ni 57% wakilinganishwa na 25% wanaotumia Chrome, 12% wanaotumia Firefox na 5% wanaotumia Safari.(BBC)
No comments:
Post a Comment