Thursday, January 14, 2016

MILIPUKO YA MABOMU YATOKEA JAKARTA (BBC)

AFPImage Maafisa wa usalama wamezingira eneo hilo

Milipuko ya mabomu imetokea katika jiji kuu la Indonesia, Jakarta na baadaye ufyatulianaji mkali wa risasi na watu watatu wanahofiwa kufariki. Milipuko imetokea maeneo kadha, ikiwa ni pamoja na mgahawani katika duka la kibiashara lililoko karibu na ikulu ya rais na afisi za UN.

Kuna ripoti za maafisa wa polisi kuonekana kwenye majengo na barabara za mji huo karibu na kituo hicho cha kibiashara. Eneo hilo limezingirwa na maafisa wa usalama. Bado haijabainika ni nani huenda amehusika katika shambulio hilo.

Indonesia, taifa lenye Waislamu wengi zaidi duniani, imeshambuliwa na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu awali.

Majuzi, imekuwa kwenye hali ya juu ya tahadhari kutokana na tishio kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State. Hili ndilo shambulio la kwanza kubwa kutokea Jakarta tangu mashambulio kwenye hoteli za Marriot na Ritz mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment