Kampuni kongwe na maarufu nchini kwa kusambaza vifaa
mbalimbali vya michezo na yenye uzoefu wa siku nyingi, imeingiza vifaa vipya na
vya kisasa kabisa vya michezo kwaajili ya wana michezo wote nchini.
Kampuni hiyo inayojushughulisha na usambazaji wa huduma hiyo
imesema lengo lake ni kuinua ubunifu na hari ya michezo nchini ili kuinua
viwango vya michezo.
Kampuni ya Isere Sports imewataka wanamichezo ikiwa ni
pamoja na wapenzi wa michezo nchini kuchangamkia vigfaa hivyo kwani ni vya
kisasa na vimetengenezwa kwa viwango vya kimataifa vyenye kuzingatia mahitaji
ya msingi ya mtumiaji.
Akizungumza na ImmaMatukio Blog, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni
hiyo Bw. Abasi Isere (kushoto), amesema anawakaribisha wa michezo haswa wana UMISETA na
UMISHIMUTA na kwamba Isere kuna kila wanachohitaji kukidhi mahitaji yao.
“Sisi tunazingatia mahitaji ya wanamichezo, ikiwa ni pamoja
na viwango vya hali ya juu ili kuwawezesha watumiaji kutumia na kufikia malengo
yao kirahisi” alisema Bw. Abasi.
Kati ya vifaa hivyo ni pamoja na jezi za soka, netball,
riadha na michezo mingine kama tenis, volleyball, n.k lakini pia kuna mipira,
filimbi, viatu , sox, na mengineyo mengi
No comments:
Post a Comment