Wednesday, May 28, 2014

BASI LA SHABIBY LANUSURIKA KUPATA AJALI, ABIRIA WAPONA



Abiria wanaosafiri kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro kutoka Dodoma wamenusurika kupata ajali baada ya basi walilokuwemo katika basi la kampuni ya Shabiby Express(Pichani), lenye namba za usajili T405BYS baada ya basi hilo kuanja njia kutokana na kupasuka tairi.

Basi hilo lilipasuka tairi ya mbele upande wa kushoto, liliacha njia na kutoka nje ya barabara umbali zaidi ya mita 100 katika eneo la Ulyampiti ikiwa ni kilometa 15 kutoka Ikungi mkoani Dodoma.


Hata hiyvo hakuna aliyejeruhiwa katika ajali hiyo, na kwamba abiria wote wako salama, mpaka tunakwenda mitamboni matengenezo ya basi hilo yalishakamilika tayari kuendelea na safari hiyo.


No comments:

Post a Comment