Monday, May 23, 2016

SERIKALI KUENDELEA KUONGEZA BAJETI KWA AJILI YA BARABARA.

Na MAELEZO, Dodoma.

SERIKALI imesema itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya barabara kadri uwezo wa kifedha utakavyoongezeka.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Miko na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum. Mhe. Sophia Mwakagenda aliyetaka kujua utayari wa Serikali katika kukubali ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya na kuongeza fedha katika Bajeti ya mwak 2016/2017.

Mhe. Jafo amesema kwamba, Halmashauri ya Rungwe iliandaaa makisio ya bajeti ya Shilingi bilioni 7.9 kwa ajili ya matenegenzo ya barabara katika bajeti ya mwaka 2016/17, hata hivyo kutokana na ukomo wa bajreti fedha zilizoidhinishwa ni shilingi milioni 920 ambazzo zitatumika kwa ajili ya matenegenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja.

"Katika mwaka wa fedha wa 2015/16, Halmashauri hiyo ilitengewa shilingi milioni 870 na tayari Serikali imeshapeleka milioni 157.9", alisema Mhe. Jafo.

Aliongeza kuwa, fedha za Mfuko wa Barabara katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 247.5 ambazo endapo zingegawanywa sawa kwa Halmashauri zote 181 zilizopo, kila Halmashauri ingekuwa na bajeti ya shilingi bilioni 1.3.

Amefafanua kuwa mara zote mahitaji yamekuwa ni makubwa kuliko uwezo wa rasilimali fedha kukidhi mahitaji hayo ndiyo maana Serikali inaweka vipaumbele ili kutekeleza mambo machache kwanza kulingana na uwezo uliopo kibajeti.

"Serikali itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya barabara kadri uwezo wa kifedha utakavyoongezeka", alisema Mhe. Jafo.

MWISHO


No comments:

Post a Comment