Tuesday, March 20, 2018

ALIYEKUWA RAIS WA UFARANSA AKAMATWA KWA KUPOKEA HELA ZA GADDAFI 2007

Aliyekuwa rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy (Pichani) amekamatwa na anashikiliwa na polisi akihojiwa kuhusiana na tuhuma za kupokea euro milioni 5 (sawa na Shilingi Bilioni 13.9) kwaajili ya kampeni mwaka 2007 kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.

Ufaransa ilifungua uchunguzi mwaka 2013 zikidai ushindi wa Sarkozy wa mwaka 2007 ulitokana na fedha zisizo halali kutoka kwa Marehemu Gaddafi.

Rafiki wa Sarkozy ambaye pia alikuwa waziri, Brice Hortefeux, naye pia amehojiwa na polisi jumanne asubuhi kuhusiana na uchunguzi huo, chanzo kingine kilichopo karibu na uchunguzi huo kileleza.

Sarkozy, alitawala Ufaransa kuanzia mwaka 2007 mpaka 2012, mar azote amekuwa akikanusha madai ya kufanya kampeni chafu na kupokea kiasi hicho cha fedha kwaajili ya kampeni na kuziita tuhuma hizo “za ajabu”

Mwezi januari mfanyabiasha wa Ufaransa aliyedaiwandiye aliyefikisha fedha hizo ili kufadhili kampeni za Sarkozy toka kwa Gaddafi, alikamatwa nchini Uingereza na kutoka kwa dhamana baada ya kufikishwa katika mahakamani jijini London.

Sarkozy ameshasimamishwa mahakamani kwa tuhuma kama hizo kuhusiana na ufadhili wa kampeni katika uchaguzi wa mwaka 2012 na kushindwa na Francois Hollande.

No comments:

Post a Comment