PICHANI: Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambayo ilifanyika kimkoa kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa Habari Jijini Tanga kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Edward Bukombe na kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (Tanga Presse Club) Hassan Hashim
WAANDISHI wa Habari Mkoani Tanga wametakiwa kuwajibika kwa kufanya kazi kwa kufuata miongozo na maadili ikiwemo kuweka uzalendo mbele kwa ajili ya maslahi ya nchi na jamii zinazowazunguka.
Hayo yalisemwa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi wakati akizungumza katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambayo ilifanyika kimkoa kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa Habari Jijini Tanga.
Alisema iwapo watazingatia maadili na kuweka mbele uzalendo itasaidia kuweza kuwasaidia kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi na maendeleo kupitia vyombo vya habari ili viweze kupata mafanikio makubwa.
“Ndugu zangu niwaambie uhuru wa habari ukitumika vyema vyombo vya habari vina mchango mkubwa kwa mkoa na nchi katika nyanja za kijamii, kiasiasa na kiuchumi kwa kujenga jamii yenye kiu ya kuleta maendeleo “Alisema.
“Lakini pia amani na utulivu wa jamii ni muhimu zaidi kuliko vipato vyote ...Gharama ya kurudisha amani ikivunjika ni kubwa kwa hiyo wote tuna wajibu wa kuilinda kwa kauli zetu, vitendo vyetu na maandishi yetu”Alisema.
Aidha alisema vyombo vya habari vina wajibu mkubwa kwenye jamii kwa kupasha habari zenye ukweli,kujenga na kuleta matumaini kwa jamii hivyo ni vema kuchuja na kuepuka habari zinazoleta migongano na mifarakano katika jamii hata kama zinavutia na kuwapa vipato vya haraka.
Hata hivyo alisema vyombo vya habari ni kiungo muhimu kati ya uongozi wa makali popote na jamii lakini pia maagizo, makatazo,fursa na taarifa mbalimbali zitokazo kwa viongozi huwafikia wananchi kupitia vyombo vya habari .
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga Lulu George kulia akifutilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edwaed Bukombe
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano huo wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Wandishi wa Habari mkoani Tanga (Tanga Presse Club) Hassan Hashim kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tanga Presse Club Lulu George anayefuatia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment