Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

Monday, May 16, 2016

WCF KUTOA MAFUNZO KWA MADAKTARI KUHUSU MAGONJWA YA KAZI

Imeelezwa kuwa ipo haja kwa vituo vya Afya hapa nchini kuwepo na wataalamu ambao watasaidia kitaaluma kubaini, kutibu na kutathimini magonjwa yatokanayo na kazi.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) Masha Mshomba wakati wa mafunzo kwa madaktari yanayohusu kubaini na kutibu magonjwa yatokanayo na kazi.

Amesema kuwa kuna kila sababu ya vituo hivyo kuwe na wataalamu ambao watasaidia kutambua na kutibu magonjwa yaokanayo na kazi ili kurahisisha masuala ya ulipaji wa fidia.

Mshomba ameeleza kuwa suala la kutambuna na kubaini magonjwa yatokanayo na kazi ni la kitaalamu zaidi na ndio maana mfuko huo umeamua kutoa mafunzo hayo kwa madaktari.

"Mafunzo haya kwa madkatari yatawasaidia kufanya tathimini ya magonjwa yatonakayo na kazi ili wawe miongoni mwa washauri wa mfuko huo,pia mafunzo haya ya awamu ya kwanza yamewashirikisha Madaktari 93 kutoka mikoa ya Dar es salaama, Morogoro, Dodoma, Lindi, Mtwara na mikoa mingine ya Pwani.

Tuesday, November 17, 2015

KIPINDUPINDU CHANYEMELEA JIJI LA MBEYA


Na Mwandishi wetu,Mbeya

Halmashauri ya jiji la Mbeya limewataka wafanyabiashara ndogondogo hususani wa chakula kujijengea tabia ya kuchoma taka nyakati za jioni mara wamalizapo kuuza biashara zao na si kusubili gari ya taka kuja kuzoa.

Aidha imewataka wakazi hao kuondokana na fikra duni ya kuamini kuwa kazi ya uzoaji wa taka na kusafisha mazingira ni ya halmashauri ya Jiji na sio mali ya mtu.
( Picha Kushoto:Wafanyabiashara ndogo ndogo katika eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiendelea na shughuli zao kama kawaida . )

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dkt. Samweli Lazaro, amesema, wananchi wanatakiwa kujenga tabia ya usafi na sio kusubili kupigizana kelele na serikali kwa kuwahimiza kufanya usafi kwani adui mkubwa wa afya ni uchafu hivyo kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa mwezake katika kutunza mazingira.


Sunday, November 15, 2015

AFYA BORA INAANZA NA KIFUNGUA KINYWA BORA - SIKU YA KISUKARI DUNIANI

Dk. Bhuvaneshwari Shankar, Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo. (KUSHOTO
 PICHANI)

Na Mwandishi Wetu,
Novemba 14 kila mwaka tunaadhimisha siku ya kisukari duniani ili kuongeza uelewa kuhusu madhara ya kisukari, matatizo yanayoletwa na huu ugonjwa na taarifa muhimu kuhusu kisukari.

Siku hii inabeba ujumbe mahususi kwa watu wote ulimwenguni. Kauli mbiu katika siku hii tokea 2014 hadi 2016 ni maisha bora na kisukari(healthy living and diabetes) na mwaka huu kuna mtazamo zaidi katika kuzingatia mlo kamili na kuanza kila siku na kifungua kinywa bora.

Kutoka katika shirika la kisukari Africa, Tanzania ni kati ya nchi 32 katika shirikisho hilo kwa viwango vya nchi zenye viwango vya kisukari duniani. Kulikuwepo na zaidi ya kesi milioni 1.7 za kisukari hapa Tanzania kwa mwaka 2014. Shirika la afya duniani (WHO) linakadiria zaidi ya watu milioni 180 ulimwenguni wana kisukari, na hiyo takwimu inatarajiwa kuongezeka ifikapo mwaka 2030 kama hamna hatua yoyote itakayochukuliwa.


Thursday, October 08, 2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA MACHO DUNIANI

Imeelezwa kuwa takribani watu 945,000 wanasumbuliwa na matatizo ya kuona kwa viwango mbalimbali hapa nchini idadi yao ikiwa ni mara tatu ya watu wasioona kabisa ambao ni takribani watu 315,000.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii idadi ya watoto wenye matatizo ya kuona duniani ni milioni 19 huku wazee wakiongoza kwa asilimia 82 pia nchi zinazoendelea zinaongoza kwa idadi kubwa ya watu wenye matatizo hayo kwa asilimia 90.

Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Dkt.Donan Mmbando,Katibu Mkuu wa wizara hiyo,ikiwa nisehemu ya kuadhimisha siku ya afya ya macho duniani yenye kauli mbiu ya "Afya bora ya macho kwa wote"yenye lengo la kuhamasisha wadau kushirikana katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za macho katika ngazi zote za utoaji huduna za afya.

Wednesday, September 16, 2015

MASK YA ASALI, NDIZI MBIVU na NDIMU kwa WALE WENYE USO WA MAFUTA

MASK YA ASALI, NDIZI MBIVU na NDIMU kwa WALE WENYE USO WA MAFUTA
Kama mlivyoomba wadau kwa wale wenye USO wenye MAFUTA mengi hii ni MASK unayoweza kutumia ukiwa nyumbani na ikakuaaidia.

Nini cha kufanya:-
1. Ponda ponda NDIZI MBIVU MOJA mpaka iwe laini kabisa
2. Chukua KIJIKO KIMOJA CHA ASALI
3. Chukua KIJIKO KIMOJA CHA NDIMU
4. Changanya kwa pamoja vitu hivyo vizuri.
5. Paka mchanganyiko huo kwenye uso msafi kama inavyoonekana kwenye picha na kaa nao kuanzia dakika 15 hadi 30 kisha osha na maji ya uvuguvugu.

Unaweza tumia mask hii mara moja kwa siku.

Imeandaliwa na Honey Spring kwa kushirikiana na Jamiimojablog, Kwa mahitaji yako ya ASALI wasiliana nasi 0683370065 au 0769129351, karibuni sana



Thursday, March 06, 2014

WHO - PUNGUZENI SUKARI, INA MADHARA MAKUBWA KIAFYA

Shirika la Afya Duniani WHO limepunguza kwa nusu kiwango cha sukari kilichopendekezwa kwa matumizi ya binadamu ili kuepusha matatizo ya kiafya kama vile kunenepa kupita kiasi na meno kuoza.
Mswada mpya wa mwongozo wa matumizi ya kila siku ya sukari umepunguza kiwango cha sukari inayopaswa kutumiwa na binadamu hadi asilimia tano ya kalori au vijiko sita vya sukari kwa siku.

WHO imesema kuwa sukari ndio chanzo cha janga la kunenepa kupita kiasi linalowahangaisha takriban watu nusu bilioni kote duniani, tatizo ambalo bado linaongezeka hususan katika mataifa yanayoendelea.(BBC)

Wednesday, July 24, 2013

WATU 1,500 WAATHIRIKA NA MSHTUKO WA MOYO


Zaidi ya watu 1,500 waathirika na mshtuko wa moyo ulio sababishwa na kushindwa kula kitu chochote asubuhi (kiamsha kinywa) , kulingana na utafiti uliofanywa nchini Marekani.

Utafiti wao uliowahusisha wanaume 27,000 ulionyesha kuwa wale wasiokula kiamsha kinywa wako katika hatari ya kupata matatizo ya moyo.

Kikundi hicho cha wataalamu katika chuo kikuu cha Havard kitivo cha afya ya umma,kilisema kuwa kukosa kiamsha kinywa kunasababisha mwili kutumia nguvu nyingi zaidi kuliko kawaida.