Thursday, November 19, 2015

ISIS YATOA PICHA YA BOMU LILILOLIPUA NDEGE YA URUSI NA KUUA ABIRIA 224

Kundi la kigaidi la Kiislam, maarufu kama ISIS limetoa picha ya bomu na kudai ndilo lililotumika kulipua ndege ya Urusi katika anga ya Misri eneo la rasi ya Sinai mwezi uliopita na kuua abiria 224 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.

Picha hiyo (KULIA) ilichapishwa katika jarida lenye msimamo mkali la kiingereza likionesha neno “EXCLUSIVE - picha ya IED iliyotumika kushusha ndege ya shirika la Urusi” 

Picha hiyo ilionesha kikopo cha kinywaji cha soda aina ya Schweppes Gold na kuambatanishwa na vitu ambayvo ni sehemu ya vilipuzi.

Taarifa hiyo iliandika “ Tarehe 30, Septemba, 2015, baada ya kuunga mkono Nusayrī tāghūt kwa miaka mingi katika vita dhidi ya Uislamu wa Shām, Urusi imeamua kushiriki moja kwa moja kwa kutumia ndege zao katika vita hiyo.
Ilikuwa ni uamuzi wa haraka usio na busara wa Urusi, kana kwamba vita kupinga Uislam wa Qawqāz halikuwa kosa la kutosha.

Baada ya kupata njia za kiusalama za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sharm el-Sheikh za kushusha ndege ya taifa linaloshirikiana mataifa yanayoongozwa na Marekani dhidi ya vita na taifa la Kiislamu, lengo likabadilika na kuwa ni ndege ya Urusi.

Bomu liliingizwa kinyemela katika ndege hiyo, na kusababisha vifo vya raia wa Urusi 269 na wengine 5 ikiwa ni miezi michache baada ya uamuzi wa Urusi” 

Hata hivyo Urusi imesema bomu lilitumika kuangusha ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria ambao wengi walikuwa ni watyalii wa Kirusi.





No comments:

Post a Comment