Friday, November 20, 2015

BUSU LA SINEMA MPYA YA JAMES BOND LAZUA UTATA NCHINI INDIA

Bodi ya Filamu nchini India imeficha baadhi ya vipande vya filamu mpya ya James Bond “007” ijulikanayo kama “SPECTRE” vinavyoonesha akipiga mabusu, hatua hiyo ni kuendana na maadili na kulinda tamaduni na mila za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN, Kiongozi wa Bodi hiyo, Pahlaj Nihalani ameliambia shirika la habari kuwa wamepunguza sehemu mbili zinazoonesha Daniel Craig(007) akimbusu Monica Bellucci pamoja na Lea Seydoux

“Kazi yetu ni kuziba maeneo yasiyofaa kutokana na daraja la sinema, kwa hiyo tumetekeleza hilo” Nihalani aliiambia AFP. Matusi mawili pia yameondolewa.

Hata hiyvo wakihojiwa na CNN, baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo walikosoa hatua hiyo. Ashok Pandit aliandika katika ukurasa wake wa Tweeter, “kimekuwa kituko cha uhuru wa watengeneza filamu.”

India ni nchi inayoficha matukio mbalimbali. Ni nchi yenye demokrasia kubwa kuliko nchi nyingi duniani, utamaduni wenye mijadala ya kisiasa ya kina pamoja na vyombo vingi vya habari.

Nchi hiyo imekuwa na historia ya kuzuia vitabu, filamu, miziki na hata ramani. Mapema mwaka huu mahakama moja nchini humo ilizuia filamu ya makala ya BBC “India’s Daughter”. Makala hiyo inaonesha mwenendo wa kesi ya ubakaji na mauaji.

Filamu nyingine ya vichekesho iliondolewa katika mtandao wa internet mwezi januari baada ya wazalishaji wa filamu hiyo kutishiwa kushtakiwa. Filamu nyingine ya "Fifty Shades of Grey" ilizuiwa kuingia katika nyumba za sinema nchini humo kutokana na picha za mapenzi.

Matukio yote hayo huusishwa na tamaduni na imani za dini. Katiba ya nchi hiyo inalinda uhuru wa kujieleza lakini kwa wale wanaonesha dharau kwa imani za dini wanaweza kuishia jela.
Uamuzi wa kuondoa vipande vya mabusu katika filamu ya Bond umeshambuliwa sana katika mitandao ya kijamii, ambapo kampeni mbalimbali zimeanzishwa.


No comments:

Post a Comment