Friday, November 20, 2015

SASA UNAWEZA ANGALIA TELEVISION KWA SIMU ZA MKONONI

Dar es Salaam, Tanzania 19 Novemba 2015, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua huduma ya ziada itakayowawezesha wateja wake nchi nzima kuangalia vipindi vya televisheni katika vituo vya ndani na nje ya nchi kupitia simu zao za mkononi.

Huduma hii mpya ijulikanayo kama "Airtel TV" imeunganishwa na vituo 8 vya televisheni vya ndani na nje ya nchi na kuwawezesha wateja wa Airtel kuangalia vipindi vilivyopita katika tamsilia wanazozipenda, kuangalia sinema na video wanazohitaji kupitia simu zao.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa "Airtel TV" Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando (PICHANI JUU)alisema "kwa kawaida mara nyingi watanzania wanaangalia vipindi vya televisheni wakiwa nyumbani wakati wa jioni baada ya kutoka katika kazi zao.

Tunazindua huduma yenye gharama nafuu itakayowawezesha wateja wetu kupata taarifa pindi wasipokuwapo majumbani mwao. "Airtel TV" itawapatia uzoefu wa kipekee na kuwahabarisha wateja wetu wakati wowote wakiwa katika shughuli zao au kwenye foleni, bila kikomo kupitia simu zao za mkononi"

" huduma hiii imelenga kukidhi mahitaji ya wateja kwa kuwapatia habari kiurahisi kwa kujiunga na kifurushi cha siku , wiki au mwezi. Tunaamini huduma hii itapunguza uwiano wa watu wasiokuwa na fursa ya kuangalia Televishoni na pia kuwawezesha kupata matukio kwa wakati kupitia simu zao mahali popote pale walipo" aliongeza Mmbando

Akiongea kuhusu mahudhui na jinsi ya kujiunga na huduma hiyo, Meneja huduma za ziada ,Prisca Tembo alieleza zaidi kuhusu dhamira yao ya kutoa huduma yenye kiwango cha juu na gharama nafuu. " tunayo furaha kuwawezesha watanzania kuangalia vipindi vya televisheni kupitia simu zao kwani tunaenda sambamba na mpango wa serikali wa kidigitali wenye lengo la kuwa na jamii kupata taarifa za yanayotokea ndani na nje ya nchi kwa wakati na kiwango cha juu.

Tembo aliongeza kwa kusema ili kupata huduma ya "Airtel TV" mteja anatakiwa kupakua au kudownload application kwa kupitia linki ya https://goo.gl/iSvaJC kwa simu za Android na https://goo.gl/IMvzCt kwa simu za IOS.

Baada ya kuzi download mteja ataweza kununua kifurushi cha internet maalum cha Televisheni kwa kupiga *148*88# tozo za kujiunga ni Tshs 499 kwa siku, Tshs 2,999 kwa wiki naTshs 11,999 kwa mwezi. Vituo vinavyopatikana katika "Airtel TV" ni pamoja na Star TV, TBC, Fight Box, 360 tune box, Citizen, FilmBox, Channel Ten na Aljazeera.


No comments:

Post a Comment