Monday, November 16, 2015

MWANAMKE AUA MJAMZITO KISHA AMPASUA NA KUTOA MTOTO

Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi nchini Mexico, baada ya kumshawishi mwanamke mjamzito kwenda nyumbani kwake kabla ya kumuua na kumpasua kisha kutoa mtoto ndani ya tumbo lake.

Nancy Carrasco (PICHANI KULIA), 34, ambaye pia alikuwa mjamzito na kisha mimba yake kuharibika miezi mitatu kabla ya kujifungua, lakini badala ya kuitaarifu familia yake, alidanganya kuwa bado ni mjamzito, linaarifu gazeti la Daily Mirror.

Licha ya uongo wake aliendelea kuhudhuria kliniki ya wajawazito kama kawaida na ndipo alikutana na mjamzito mwingine, Luviniydi Yasmin Velazques Thomas mwenye umri wa miaka 23, na kuanza urafiki naye.

SOMA ZAIDI. . .


Baada ya urafiki wao kupamba moto, Nancy alimualika Yasmin nyumbani kwake huko Tijuana, eneo la Mexico lililoko karibu na mpaka wa Marekani, ambapo alimuua na kumpasua kisha kumtoa mtoto.

Kwa mujibu wa poilisi, Nancy akijitahidi kumwokoa mtoto asife, alikimbia katika hospitali ya kujifungua ya IMSS na kudai kuwa mtoto ni wa kwake.
Hata hivyo madaktari wanadai hakuwa na dalili zozote za kutoka kujifungua, hivyo waliwasiliana na familia yake wakidai mfuko wa uzazi (placenta) upelekwe hospitali hapo.  Ndugu hao walipofika nyumbani kwake, walishtuka kukuta mwili wa mwanamke na ndipo walipotoa taarifa polisi.

Nancy alipobanwa na kuhojiwa kuhusu mwili huo, polisi wanasema alikubali na kusema “nimemtoa mtoto wake na kumuua. Nilimkaba kwa nyuma kwa kutumia mtandio wake. Kisha nikatumia kisu kumpasua tumbo lake na kisha kumuibia mwanae.”

Alidai sababu ya kufanya yote hayo ni hofu kuwa mumewe angemuacha kama angegundua kuwa mimba yake iliharibika.







No comments:

Post a Comment