Monday, November 23, 2015

ARUSHA SASA KUFURAHIA INTANETI YA KASI ZAIDI KUTOKA TIGO

Arusha, Novemba 18 2015. Wateja wa Tigo waishio Arusha sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.

‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es Salaam kuanzia mapema mwaka huu’’, amesema Mkuu wa Kitengo cha Internet David Zacharia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Zacharia amesema: "ni kielelezo cha jinsi ambavyo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya dijitali katika maisha ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia teknolojia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania."
Mtandao wa 4G LTE una kasi kubwa zaidi katika kuperuzi na kupakua kwa rahisi kutoka kwenye mtandao wa intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma hii pia inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia ya mtandao.

“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waishio Arusha kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na Intaneti yenye kasi zaidi,” Gutierrez amesema. Arusha ni makao makuu ya taasisi nyingi za kimataifa ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki na kitovu cha utalii nchini.

Wateja wote wa Tigo 4G LTE watanufaika na promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama bonasí.

Ametaja miji mingine katika mikoa sita ambapo 4G itaanza kupatikana hivi karibuni kuwa ni Arusha, Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza na Tanga, “jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G nchini Tanzania.” Lengo kuu ni kufkisha huduma ya 4G katika kila kona za nchi ifikapo mwaka ujao, Zacharia ameongeza kusema.


Mshereheshaji wa hafla MC Taji Liundi akitoa maelekezo jinsi intaneti ya kasi zaidi kutoka Tigo katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita


Wadau Husni na Benedict Mponzi wakiwa katika pozi katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita


Watoa huduma wa Tigo wakiwa katika pozi tayari kutoa msaada na maelekezo jinsi gani wateja wa TIgo wa jijini Arusha na maeneo ya jirani watakavyofurahia intaneti ya kasi hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita


Mkuu wa kitengo cha biashara wa Tigo Bw, Shavkat Berdiev akitoa hotuba fupi katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita



Wageni rasmi wakipiga ngoma kama kuashiria uzinduzi rasmi w a Intaneti ya kasi zaidi nchini ya TIGO 4G lte katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita


Watoa huduma wa Tigo mkoani Arusha wakiwa katika pozi na tayari kutoa huduma na maelekezo jinsi huduma ya Tigo 4G lte itakavyowanufaisha wakazi wa jiji la Arusha na maeneo ya jirani katika hafla iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita


Mtaalamu wa mitandao ya kijamii wa Tigo , Bi Samira Baamar akiwa na washindi wa zawadi za vifaa vya intanet vinavyotumia teknolojia ya 4g lte (MODEM NA ROUTER ) waliofanikiwa kujishindia katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita


Mgeni rasmi Wilson E Nkambaku , mkuu wa wilaya Arumeru akitoa hotuba fupi katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita


Umati wa wakazi wa jiji la Arusha wakifurahia jambo katika katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita












No comments:

Post a Comment