Monday, November 23, 2015

JAMAA ALIYEBADILI JINSIA AJIUA, KISA KAHUKUMIWA KWENDA JELA YA WANAUME

Mwanaume aliyebadili jinsia na kuwa mwanamke aliyetishia kujiua iwapo angepelekwa jela ya wanaume, amekutwa amekufa. Vicky Thompson (PICHANI KULIA), mwenye umbra wa miaka 21, alihukumiwa kifungo cha miezi 12 katika jela ya HMP Leeds baada ya kuvunja makubaliano ya hukumu aliyopewa awali.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror la niching Uingereza, Mwanasheria wa Vicky, Mohammed Hussain alimweleza hakimu kuwa Vicky ni mwanamke na kumtaka ampeleke kutumikia kifungo chake katika mahakama ya New Hall kitengo cha wanawake, karibu na Wakefield.

Gazeti la Daily Mirror lilieleza kuwa Vicky ambaye bado alikuwa hajabadilishwa maungo yake kwa njia ya upasuaji, alikerwa sana na kitendo cha kufungwa katika jela ya wanaume na kutahadharisha kuwa angejiua.

Hata hivyo sheria za magereza nchini Uingereza zinasema wazi kuwa, mshtakiwa atatumikia kifungo katika jela kutokana na jinsia yake. “ na kwa mujibu wa sheria za nchini Uingereza” hiyo ni kumaanisha kutokana na jinsia iliyoandikwa katika cheti cha kuzaliwa.

Vicky Thompson mkazi wa Keighley, West York nchini Uingereza amekuwa akijitambilisha kama mwanamke tokea akiwa mdogo lakini hakuwahi kufanyiwa upasuaji kubadilisha maungo yake.

No comments:

Post a Comment