Wednesday, November 25, 2015

BINTI ALIYEJIUNGA ISIS APIGWA MPAKA KUFA ALIPOJARIBU KUTOROKA

Samra Kesinovic, 17, pichani kushoto aliondoka Austria mnamo 2014 mwezi aprili akiwa na rafiki yake Sabrina Selimovic, imedaiwa amepigwa na magaidi wa kundi la magaidi wa Kiislam wa ISIS mpaka kupoteza maisha wakati alipojaribu kutoroka eneo la Raqqa.

Inaaminika kuwa Sabina alifariki mwezi disemba mwaka jana wakati wa kipindi cha mapigano makali. Wasichana hao wawili walionekana katika video ya propaganda za ISIS mda mfupi baada ya kuwasili nchini Syria. Rafiki yake ambaye waliambatana aliuwawa miezi michache kabla yake.

Samra Kesinovic na rafiki yake Sabina Selimovic(kulia) wakiwa katika picha iliyopigwa na kundi la magaidi wa ISIS mda mfupi baada ya kuwasili nchini Syria mwezi aprili 2014.
Magazeti kadhaa ya Australia yameripoti kwamba Samra alipigwa mpaka kupoteza maisha alipokuwa akijaribu kutoroka Raqqa.

Pamoja na kwamba maafisa wa serikali wamegoma kuongelea suala hilo.

Wasichana hao wawili wenye asili ya Viena wakiwa na umri wa miaka 17,16 ambao wazazi wao wote wawili ni wakimbizi wa Bosnia, walipotea mwezi aprili mwaka jana, kwa madai kuwa wanataka kwenda kupigana vita nchini Syria.

Kwa mujibu wa gazeti la The Local lililomkariri mwanamke mmoja raia wa Tunisia aliyekuwa anaishi na wasichana hao katika kambi ya Raqqa, ambaye pia hakutaka kutajwa jina lake, alidai kuwa alifanikiwa kutoroka kambi ya ISIS.

Mapema mwaka huu, maafisa wa Umoja wa Mataifa waliripoti kuwa wasichana wawili wenye asili ya Austria wenye makazi yao Vienna wamedhibitishwa kufa katika mapigano.

Kwanza walikwenda katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara kwa ndege, baadae walielekea kusini mwa Uturuki katika mji wa Adana. Baada ya hapo walipotelea kusiko julikana.

Badala yake walionekana katika mitandao ya kijamii wakionekana na mabunduki huku wamezungukwa na watu wenye silaa, picha zilizoonesha kutumiwa kwaajili ya kuvutia utafuta wasichana ambao wangejiunga na kundi hilo.







No comments:

Post a Comment