Wednesday, November 18, 2015

MAMA ADAI MZIMU WA MICHAEL JACKSON UMEMPA MIMBA, AFUNGUA KESI

Mwanamke mmoja ameibuka na madai kuwa amejifungua mtoto wa mzimu wa Michael Jackson. Mwanamke huyo amefungua kesi kuishitaki wamiliki wa mali za mkongwe huyo wa muziki wa Pop ili kupata fidia ya matunzo ya mtoto.

Kwa mujibu wa chaneli ya televisheni ya shirika la Now8News nchini Marekani, Kiera Johnson (Pichani Kushoto) alidai kuwa wakati anaangalia dvd ya saa mbili ya toleo maalumu la miaka 30 ya Michael Jackson (Michael Jackson 30 Year Anniversary Special), lipofikia sehemu ya muziki wa Thriller, macho yake yakawa mazito akasinzia. Na ndio hapo sasa maajabu yalipotokea…


Kiera, 32, anaeleza “ghafla, niliamshwa na mkono uliokuwa unanipapasa usoni wakati nilikuwa ndani peke yangu, mume wangu akiwa kazini. Kilichofuata nilikuwa nalazimishwa kufanya mapenzi na Michael Jackson.

Hata hivyo hakuwa Michael Jackson mweupe, alikuwa mweusi na amevalia kama ametoka kwenye video ya nyimbo hiyo. Nilijaribu kumzuia na kumwambia ‘stop’ lakini hakusikiliza.”

Kiera alidharau tukio hilo kwa madai kuwa ilikuwa ni ndoto tu. Hata hivyo tarehe 25 septemba, 2015 yeye na mumewe (wote wazungu) walipata mtoto wa tatu wa kiume.

“Kila kitu kimeenda vizuri” alisema mume wa Kiera, Ken. “lakini nilipomuona mtoto wangu kuwa ni mweusi, nikasema ‘ni kitu gani hiki!’ nilikumbwa na mshtuko mkubwa. Na ndipo Kiera aliponieleza kuhusu ndoto yake ya ajabu.

“nafikiri si sahihi, ndio maana tunashitaki wamiliki wa mali za Michael Jackson. Tunachotaka ni fedha za kutosha kusaidia malezi ya mtoto wake” alieleza baba huyo.

Kiera amedai hakuwahi kuchepuka hata siku moja toka awe na Ken, wachilia mbali na mtu mwenye utaifa mwingine. Nae Ken anaemtambulisha Kiera kama “Malkia” wake anasema anamuamini sana mkewe.

Familia hiyo inasema ikotayari kumalizana nje ya mahakama na wameipa familia ya Michael Jackson mpaka tarehe mosi januari 2016 kutoa jibu. Familia ya Jackson haijasema chochote hadharani kufuatia tuhuma hizo.






No comments:

Post a Comment