Tuesday, November 17, 2015

MKUTANO WA UMEME AFRIKA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkutano wa mwaka maarufu kama POWERING AFRICA: Tanzania Investment Conference (www.PoweringAfrica-Tanzania.com) unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro Hotel kwa siku mbili kuanzia tarehe 3 mwezi Disemba 2015.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kusambazwa na mtandao wa African Press Organisation mapema leo, mkutano huo utaangazia masuala ya umeme wa Tanzania baada ya uchaguzi, fursa za uwekezaji pamoja na kujenga mahusiano baina ya serikali na sekta binafsi katika soko la umeme.
Akidhibitisha taarifa hizo, January Makamba ambaye ni Mbunge Mteule wa Bumbuli, na mwakilishi kutoka tume maalumu ya Rais (President’s Delivery Bureau –PDB ), Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya Usambazaji Gesi (GASCO), walionesha dhamira ya serikali katika kukuza sekta ya nishati kama uti wa mgongo wa maendeleo nchini.

Mpaka sasa kuna makampuni 37 kutoka sekta binafsi nchini ambayo yamedhibitisha kushiriki ambayo ni pamoja na Tanzania Investment Bank, Standard Chartered Bank, Mitsubishi Corporation, Citibank Tanzania Limited, BVI Consulting, Liquefied NG Tanzania Limited, Statoil na Sunfunder.

Ajenda kuu ya mkutano huo itahusisha pamoja na dhamira ya Tanzania katika mageuzi ya nishati, kukua kwa sekta ya nishati, maendeleo ya gesi nchini, mikakati ya manunuzi ya serikali na umuhimu wa umeme katika sekta ya kilimo.

Kufuatia msaada uliotolewa na IFC ili kuwezesha utekelezaji wa maendeleo ya nishati nchini, ratiba hiyo itahusisha uwezekano wa nishati mbadala ikiwa ni pamoja na umeme utokanao na nguvu za jua, upepo, jotoardhi, na maji.





No comments:

Post a Comment