Tuesday, November 17, 2015

BREAKING NEWS: MAKOPO YA BIA 48,000 ZA PEPSI ZAKAMATWA

Jamaa mmoja amenaswa nchini Saudi Arabia, wakati akijaribu kuingiza nchini humo zaidi ya makopo 48,000 ya bia aina ya Heineken, yaliyozibwa na kufanana na soda aina ya Pepsi (PICHANI KULIA), katika taifa hilo la kiislam lililoko Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu.

Pamoja na kuwa adhabu za makosa kama hayo hutofautiana ni kinyume cha sheria kukutwa na pombe katika Ufalme wa Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa Mtandao wa LBC America, maafisa ushuru katika mpaka wa Al Batha walikamata shehena hiyo ilipokuwa ikijaribu kupenya na kuingia nchini humo.


“Gari lililobeba iliyodhaniwa kuwa na shehena ya vinywaji vya Pepsi lilisimamishwa na baada ya utaratibu wa kawaida wa kukagua bidhaa hiyo ilibainika kuwa ni pombe iliyovalishwa stika ya ilizibwa na karatasi ya Pepsi” alikaririwa akisema Meneja Mkuu wa mpaka wa Al Batha, Abdulrahman al-Mahna

Afisa huyo pia alikaririwa akisema kuwa pamoja na jitihada, ubunifu na ujanja wa kuingiza bidhaa nyingi zilizopigwa marufuku, askari doria wake “siku zote wako tayari kukamata bidhaa hizo”

Hata hivyo haijajulikana bado mtuhumiwa huyo atachukuliwa hatua gani kwa kitendo hicho.




No comments:

Post a Comment