Friday, November 27, 2015

TANZIA:MKURUGENZI MSAIDIZI WA BUNGE HELLEN MBEBA AMEFARIKI DUNIA

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36)(Pichani kulia), aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi-Shughuli za Bunge, kilichotokea ghafla leo Ijumaa tarehe 27/11/2015 wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.

Msiba upo nyumbani kwake eneo la Kisasa, Mjini Dodoma. Taarifa zaidi na taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na ratiba kamili ya maziko zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu pindi mipango itakapokamilika.

MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI AMEN

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
Dar es Salaam
27.11.2015

No comments:

Post a Comment