Tuesday, April 24, 2012

JK Uso kwa Uso na Bi Banda

Mazungumzo na Rais wa Malawi, Bibi Joyce Banda, wilayani Thylo, Blantyre jana (Aprili 23, 2012) asubuhi. kama Rais Kikwete alivyopost kwenye twitter leo

Lulu Amwaga Chozi Mahakamani


Na Mwandishi Wetu

MSANII maarufu wa filamu nchini Elizabert Michael 'Lulu' jana alimwaga chozi Mahakamani wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Msanii huyo alimwaga chozi hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na msukumano kati ya askali magereza na wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari walikuwa wakitaka kumpiga picha.

Waapigapicha hao walikuwa wanampiga picha Lulu wakati akitokea katika gari la magereza aliloletwa nalo na kupandishwa mahakamani ambapo askali magereza waliweka ulinzi mkali uliofanya wapigapicha wasipate nafasi nzuri ya kufanya kazi yao.

Hali hiyo ilileta tafrani na msukumano mkubwa na kumfanya Lulu aliyekuwa akisindikizwa na askali wa kike zaidi ya watano kuwa katika wakati mgumu ambapo hadi anafika kizimbani alionekana akitokwa na machozi.

Baada ya kufikishwa mahakamani hapo,wakili wa serikali Elizabert Kaganda,mbele ya Hakimu Lita Tarimo aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika.

Kutokana na hali hiyo aliiomba mahakama hiyo itowe tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa ambayo ni Mei 7 mwaka huu.

Kaganda baada ya hakimu kutoa tarehe hiyo,aliiomba mahakam hiyo itoe amri ya watu waliokuwa katika kordo za mahakam hiyo kupungua ili mshtakiwa huyo atoke kwa usalama.

"Mheshimiwa hakimu naomba mahakama yako itoe ami ya watu kupungua  ili mshtakiwa aweze kupita kwa ulinzi na usalama kwasababu ameingia ka kusukumwa sukumwa kutokana na watu kuwa wengi"alidai Kaganda.

Tarimo hakuwa na pingamizi na ombi hilo na kuwaamuru maaskali walio mahakamani hapo kuondoioa watu wote wasiohusika ili mshtakiwa apite kwa ulinzi na usalama.

Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 3:06 asubuhi katika akiwa ndani ya basi dogo la kijani la magereza kaiwa mshtakiwa pekee katika basi hilo pamoja na maaskali magereza.

Katika msafara huo,Lulu alisindikizwa na magari matatu likiwemo aina ya civilian STK 3058 lililokuwa limejaa askali wa kutuliza ghasia waliokuwa wakiwa na virungu pamoja na ngao.

Lulu anatetewa na mawakili watatu ambao ni Peter Kibatala,Keneld Fungamtama,Fulges Masawe na Kamishna wa Haki za Binadamu.


Picha Za Lulu Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kifo cha Kanumba



Elizabeth Michael akiwa chini ya ulinzi mkali akielekea mahakamani kusikiliza kesi yake ikitajwa kwa mara ya kwanza ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka May 7 mwaka huu

Dkt Shein Akutana na Wawakilishi wa Wafanyakazi


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar,waliofika Ikulu Mjini Zanzibar jana.[Picha na Ikulu Zanzibar.]

JK Amfariji Mke wa Marehemu Mutharika

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Malawi, marehemu Profesa Bingu wa Mutharika,wakati wa mazishi yaliyofanyika shambani kwa marehemu Ndata,wilayni Thyolo leo 


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa Marehemu Rais Wa Malawi Bingu wa Mutharika, Bi Calista Mutharika wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwa marehemu Ndata,Wilayni Thyolo, nje ya jiji la Blantyire, Malawi leo.

Picha kwa hisani ya Ikulu


Thursday, April 19, 2012

Seif na Hamad Wakutana

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Hamad Sharif  ambaye pia ni Katibu mkuu wa CUF ,akisalimiana na hasimu wake mkubwa ambaye ni Mbunge jimbo la  Wawi, Hamadi Rashid walipokutana Ikulu jijini Dar es Salaam hivi karibuni  wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa kamati ya kuratibu maoni ya Katiba.

Rais wa Zanzibar Aendelea na Ziara Pemba

 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa madarasa mapya ya kusomea katika skulimya Ukutini Kusini Pemba akiwa katika ziara mkoani humo jana.

Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akitembelea maeneo ya Skuli ya ukutini baada ya kuzinduzi wa madarasa mapya ya kusomea katika skulimya Ukutini Kusini Pemba akiwa katika ziara mkoani humo jana.

Bobby Ricketts in Dar




Magufuli Alazwa, Mtevu Anusurika



 John Magufuli Alazwa, Abbasi Mtemvu Apata Ajali

Na Mwandishi Wetu Dodoma

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli(pichani juu kulia), amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kufikishwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu  

Naibu Spika wa Bunge, Bw Job Ndugai, alitoa taarifa hiyo muda mfupi kabla ya kuahirisha Bunge jana mchana ambapo wabunge walishikwa na taharuki baada ya kusikia taarifa hiyo. 

Alisema hadi jana afya ya Waziri Magufuli ilikuwa inaendelea vizuri kutokana na matibabu aliyopewa na kuwaomba watanzania waendelee kumuombea ili apone haraka.   “ asubuhi zililetwa taarifa hapa, kwamba mwenzetu Dk. Magufuli anaumwa na amekimbizwa katika Hospitali ya Mkoa Dodoma kwa matibabu”alisema Bw Ndugai.  

“Taarifa nilizonazo ni kwamba, alipofikishwa hospitalini na kupimwa, ilionekana ‘preasure’ (shinikizo la damu) lilikuwa juu.   Alisema kuwa tayari Waziri Mkuu,Mizengo Pinda alikwenda kumjulia hali hospitalini na kueleza kuwa hali yake inaendelea vizuri, preasure imeshuka ila bado anaendelea kusumbuliwa na vichomi.  

Aidha Naibu Spika pia aliliambia Bunge, kuwa Mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu (CCM)(pichani chini kulia), amepata ajali ya barabarani mkoani Morogoro.   Alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 12.15 asubuhi baada ya gari la mbunge huyo kugongwa na roli alipokuwa akitoka Mjini Dodoma kuelekea jijini Dar es Salaam.  

Kwa mujibu wa Naibu Spika, Mtemvu na dereva wake walipata majeraha na kutibiwa mkoani humo kabla ya kuendelea na safari kuelekea Jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Katika ajali hiyo, alisema gari la Mtemvu liliharibiwa vibaya.


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA DINI LA WAISLAMU NA WAKRISTO JIJINI DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini alipowasili kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kufungua Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza leo Aprili 18, 2012.

 Baadhi ya Viongozi wa Dini wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipofika kufungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza leo Aprili 18, 2012 kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Viongozi wa Dini wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipofika kufungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza leo Aprili 18, 2012 kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo lililoanza leo Aprili 18, kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

                                              Picha Zote kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Waziri Mkuu na Mbunge wa Arumeru Mashariki

Waziri Mkuu  Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki ,  Joshua Nassari kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 18,2012.

Rais wa Zanibar Akiwa Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Watoto mara baada ya kuzindua Msikiti Masjid Raudha katika shehia ya Kiuyu Maungweni,pamoja na kuzungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Shehia hiyo jana,katika jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akishiriki katika upandaji wa miche ya Mikarafuu,katika shamba la Mikindani ,Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya Mkoani humo.

                                                     Picha Zote na Ikulu ya Zanzibar

Wednesday, April 18, 2012

Gazeti la Majira Leo...




Kituo cha Usalama

Kituo cha Polisi Kigogo, hapa ndio watuhumiwa wa uhalifu wanapohifadhiwa na mashtaka yanapopelekwa.

Boda boda Zina Vutana. . .

 Kamera yetu imenasa tukio la kushangaza eti hawa jamaa wanavutana tena kwa mpira, hawaogopi ajali wala nini, ndo maana watu wanawaponda sana Bodaboda. Juzi mtaa wa Samora, jijini Dar es Salaam. Chini inaonyesha kazi hiyo si rahisi, mpira huo umewapa taabu.




Mfanyakazi wa Ng'ombe Karudi

Hapa mheshimiwa karudi na majani ya kutosha tu kulisha ng'ombe akisubiri afunguliwe geti, siku hizi ng'ombe ni wavivu sana wameajiri binadamu wawatumikie, inabidi waletewe chakula, mavi yao yazolewe, waogeshwe...nk tofauti na miaka ya nyuma, kweli maisha yamebadilika. Hapa ni Mikocheni kati ya Business na Kwa Warioba.

Ujumbe wa Biashara wa Leo

Huyu binti wa Kimasai anauza Ugoro, hivi ugoro unakubalika eh...?!, Mwenge karibu na sokoni

Mpaka Litembee Hilo. . .

Kijana akijitahidi kulifufua gari lilichoka, Msasani Bonde la Mpunga, hivi karibuni, siku chache baadae gari hilo lilikutwa limenyofolewa karibu kila kitu na kubaki kama skrepa

Usalama Hatari

Sina uhakika kama suala la usalama jijini Dar es Salaam ni kitu kinaeleweka, nafikiri ni muhimu tuwaelimishe ndugu zetu kuhusu usalama. Hapa jamaa wananing'inia kwenye gari lilikuwa linakwenda kasi katika barabara ya Morogoro hivi karibuni maeneo ya Magomeni Kagera.

Pilika Pilika Za Jijini Dar

Jiji letu na pilika pilika zake, hapa ni maeneo ya round about ya Azam karibu na Posta Mpya

Huu Ndio Usongo Wa Elimu...

Watoto Shabani Ramadhani (kulia) na Ibrahimu Bassu (kushoto) wanaosoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Ushirika manispaa ya Shinyanga wakionesha kuwa na hamu kubwa ya elimu, hapa walinaswa na kamera yetu wakiandika kitu ndani ya daftari bila kujali walikuwa barabarani. 
                                                            (Picha na Hisani ya Majira)

Nyumba Zavunjwa Geita


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Lwamgasa,wilayani Geita wakivunja nyumba zao  jana ,kwa kile kilichoelezwa kupisha upanuzi wa barabara ikiwa ni agizo la serikali ya kijiji hicho.Zaidi ya nyumba 100 zimevunjwa ambapo familia za watu hao baadhi zinahifadhiwa kwa ndugu jamaa na marafiki na zingine kulala nje.(picha na Faida Muyomba


Ngumi Za 'Kulipwa' Za Bure...

 Jamaa wakitiana adabu mtaani, hii imetokea juzi Kawe eneo la LUKU

 Hapa jamaa wakienjoy kuona wenzao wanapigana kabla ya kuwaamulia, walisikika wengine wakidai waachwe wafundishane

Baada ya shinikizo jamaa wakaamua kukatisha pambano hilo kwa kuwaamulia

Rais Kikwete Akiwa Brazil


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012 katika mkutano wa Open Government Partnership 

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu wa Georgie Mh Nika Gilauri   katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012 baada ya kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership

  Wajumbe wa Tanzania kutoka taasisi mbalimbali za kiraia na serikali wakiwa katika  ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mabalozi wa nchi mbalimbali wakati wa Mchapalo ulioandaliwa na Balozi wa Tanzania nchini Brazil Mh Francis Malambugi nyumbani kwa Balozi usiku wa April 17, 2012 jijini Brasilia, Brazil


PICHA NA IKULU  


Thursday, April 12, 2012

Ushabiki Hatari, Kanywa Sumu Sababu ya Kanumba


Picha zikimuonyesha msichana Mariam Elias akiwa kwenye hospitali ya Tumbi wilayani Kibaha 
alikolazwa baada ya kunywa sumu ya panya akitaka kujiua baada ya kusikia msanii Steven 
Kanumba kafariki


Thursday, April 05, 2012

Rais wa Zanzibar Awaapisha Mawaziri

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri aliowaapisha waliosimama,hafla hiyo ilifanyika jana Ikulu Mjini Zanzibar,wengine Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif,(kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kulia)

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ali Juma Shamuhuna,kuwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana,kabla Shamuhuna,alikuwa Waziri wa Ardhi,Makaazi Maji na Nishati.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akimuapisha Mhe,Mansour Yussuf Himid,kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri 
asiyekuwa na Wizara Maalum,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana.
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akimuapisha Mhe,Ramadhan Abdalla Shaaban,kuwa  Waziri wa Ardhi.Makaazi,Maji na 
Nishati,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana,kabla Shaaban,alikuwa 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akimuapisha Bw Sheha Mohamed Sheha,kuwa Mshauri wa Rais-Pemba,katika hafla 
iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana.

Picha Zote na Ikulu ya Zanzibar


Joto la jiji la Dar es Salaam...

Madereva taxi wakiwa katika hali mbaya wamejihifadhi kwenye buti za magari yao kujizuia jua kali wakati wanasubiri abiria kama wanavyoonekana katikati ya jiji la Dar es Salaam mtaa wa Samora juzi. Pamoja na kwamba huu ni msimu wa mvua, mawingu mazito yamekuwa yakitanda angani lakini mvua kutokunyesha.

Mihogo Inavyosafirishwa

Mihogo ikiwa safarini kuelekea sokoni, huku waheshmiwa wakiwa wamekalia au wanalinda maana mjini hapahaminiki hivi karibuni katika barabara ya Mikumi eneo la Magomeni hivi karibuni

Wednesday, April 04, 2012

Mwisho wa upigaji kura Tuzo za Muziki Tanzania


Afisa kutoka Kampuni ya uhakiki wa mahesabu ya Innovex, Edna Masalu akieleza juu ya utaratibu wa kupiga kura kwenye tunzo za muziki Tanzania wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA. Katikati ni Lloyd Zhungu kutoka Innovex na Mratibu wa Jukwaa hilo, Agnes Kimwaga.

Mratibu wa Tunzo za Muziki Tanzania kutoka BASATA, Bw. Angelo Luhala akisistiza jambo kuhusu tunzo hizo. Pamoja na mambo mengine alitoa wito kwa watanzania kuziona tunzo hizo kama kitu chao wanachopaswa kujivunia.
 
Msanii Khamisi Ramadhan aka H Baba naye alikuwa miongoni mwa wadau wa Jukwaa la Sanaa waliotoa maoni yao kuhusu zoezi la upigaji kura kwenye tunzo za muziki Tanzania.
Mzee Rashid Masimbi ambaye ni moja ya wadau wanaoheshimika kwenye tasnia ya Sanaa nchini akitoa maelekezo na ufafanuzi kuhusu tuzo za muziki huku wadau wakimsikiliza kwa umakini.