Tuesday, April 24, 2012

Lulu Amwaga Chozi Mahakamani


Na Mwandishi Wetu

MSANII maarufu wa filamu nchini Elizabert Michael 'Lulu' jana alimwaga chozi Mahakamani wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Msanii huyo alimwaga chozi hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na msukumano kati ya askali magereza na wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari walikuwa wakitaka kumpiga picha.

Waapigapicha hao walikuwa wanampiga picha Lulu wakati akitokea katika gari la magereza aliloletwa nalo na kupandishwa mahakamani ambapo askali magereza waliweka ulinzi mkali uliofanya wapigapicha wasipate nafasi nzuri ya kufanya kazi yao.

Hali hiyo ilileta tafrani na msukumano mkubwa na kumfanya Lulu aliyekuwa akisindikizwa na askali wa kike zaidi ya watano kuwa katika wakati mgumu ambapo hadi anafika kizimbani alionekana akitokwa na machozi.

Baada ya kufikishwa mahakamani hapo,wakili wa serikali Elizabert Kaganda,mbele ya Hakimu Lita Tarimo aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika.

Kutokana na hali hiyo aliiomba mahakama hiyo itowe tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa ambayo ni Mei 7 mwaka huu.

Kaganda baada ya hakimu kutoa tarehe hiyo,aliiomba mahakam hiyo itoe amri ya watu waliokuwa katika kordo za mahakam hiyo kupungua ili mshtakiwa huyo atoke kwa usalama.

"Mheshimiwa hakimu naomba mahakama yako itoe ami ya watu kupungua  ili mshtakiwa aweze kupita kwa ulinzi na usalama kwasababu ameingia ka kusukumwa sukumwa kutokana na watu kuwa wengi"alidai Kaganda.

Tarimo hakuwa na pingamizi na ombi hilo na kuwaamuru maaskali walio mahakamani hapo kuondoioa watu wote wasiohusika ili mshtakiwa apite kwa ulinzi na usalama.

Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 3:06 asubuhi katika akiwa ndani ya basi dogo la kijani la magereza kaiwa mshtakiwa pekee katika basi hilo pamoja na maaskali magereza.

Katika msafara huo,Lulu alisindikizwa na magari matatu likiwemo aina ya civilian STK 3058 lililokuwa limejaa askali wa kutuliza ghasia waliokuwa wakiwa na virungu pamoja na ngao.

Lulu anatetewa na mawakili watatu ambao ni Peter Kibatala,Keneld Fungamtama,Fulges Masawe na Kamishna wa Haki za Binadamu.


No comments:

Post a Comment