Wednesday, April 04, 2012

Mwisho wa upigaji kura Tuzo za Muziki Tanzania


Afisa kutoka Kampuni ya uhakiki wa mahesabu ya Innovex, Edna Masalu akieleza juu ya utaratibu wa kupiga kura kwenye tunzo za muziki Tanzania wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA. Katikati ni Lloyd Zhungu kutoka Innovex na Mratibu wa Jukwaa hilo, Agnes Kimwaga.

Mratibu wa Tunzo za Muziki Tanzania kutoka BASATA, Bw. Angelo Luhala akisistiza jambo kuhusu tunzo hizo. Pamoja na mambo mengine alitoa wito kwa watanzania kuziona tunzo hizo kama kitu chao wanachopaswa kujivunia.
 
Msanii Khamisi Ramadhan aka H Baba naye alikuwa miongoni mwa wadau wa Jukwaa la Sanaa waliotoa maoni yao kuhusu zoezi la upigaji kura kwenye tunzo za muziki Tanzania.
Mzee Rashid Masimbi ambaye ni moja ya wadau wanaoheshimika kwenye tasnia ya Sanaa nchini akitoa maelekezo na ufafanuzi kuhusu tuzo za muziki huku wadau wakimsikiliza kwa umakini.

No comments:

Post a Comment