MKAZI mmoja mwanamke wa mjini Guizhou Kusini na China, ambaye hakuweza kufahamika jina lake amenusurika kufa katika ajali ya gari, lililokuwa limembeba huku akiwa hajafunga mkanda, baada kichwa chake kugonga kioo cha mbele ambacho kilimzuia asitoke nje ya gari hilo.
Abiria huyo na dareva wake walinusurika kimaajabu kufa kutokana na gari hilo kugonga nyuma ya lori lililokuwa mbele ya gari hilo na kichwa chake kugonga kioo hicho.
Baada ya kutokea ajali hiyo, kichwa cha abiria huyo kilivunja kioo na shingo yake kutokeza kwa nje huku sehemu ya mabega yake ikiwa ndani, lakini kwa bahati nzuri kilimzuia, kitu ambacho kilimsaidia kuchomoka nje ya gari.
Jeshi la zimamoto baada ya kupata taarifa za ajali hiyo lilikwenda katika eneo la tukio na kumuondoa dereva aliyekuwa amepoteza fahamu, kabla ya kumuokoa abiria ambaye shingo yake ilikuwa imezama katika kioo hicho cha mbele.
Hata hivyo kwa mujibu wa madaktari abiria na dereva wake hali zao si mbaya na wanaendelea na matibabu hospitalini.
No comments:
Post a Comment