Thursday, April 05, 2012

Rais wa Zanzibar Awaapisha Mawaziri

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri aliowaapisha waliosimama,hafla hiyo ilifanyika jana Ikulu Mjini Zanzibar,wengine Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif,(kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kulia)

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ali Juma Shamuhuna,kuwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana,kabla Shamuhuna,alikuwa Waziri wa Ardhi,Makaazi Maji na Nishati.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akimuapisha Mhe,Mansour Yussuf Himid,kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri 
asiyekuwa na Wizara Maalum,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana.
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akimuapisha Mhe,Ramadhan Abdalla Shaaban,kuwa  Waziri wa Ardhi.Makaazi,Maji na 
Nishati,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana,kabla Shaaban,alikuwa 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akimuapisha Bw Sheha Mohamed Sheha,kuwa Mshauri wa Rais-Pemba,katika hafla 
iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana.

Picha Zote na Ikulu ya Zanzibar


No comments:

Post a Comment