Wednesday, May 31, 2017

TBS YAWASHAURI WAZALISHAJI WADOGO WADOGO WA BIDHAA KUTUMIA FURSA YA BURE YA UKAGUZI


Wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa nchini wameshauriwa kutumia fursa ya bure ya ukaguzi wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania TBS.

Hayo yamesemwa na Afisa Masoko Mwandamizi kutoka katika shirika hilo,Gladnes Kaseka (pichani kushoto juu) wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya tano ya biashara ya Mkoa wa Tanga .

Alisema kuwa licha ya TBS kutoa fursa hiyo lakini bado wazalishaji wadogo na wakati wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.

"Bado wazalishaji wetu wengi hawajaweza kuifikia fursa hiyo ambayo itaweza kuwasaidia kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza kuingiza bidhaa zao kwa urahisi katika masoko ya ushindani tofauti na sasa" alisema Kaseka.


Tuesday, May 30, 2017

NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUWEKEZA KATIKA KILIMO


PICHANI: Meneja wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB), Daniel Otunge, akizungumza wakati akitoa mada kwenye semina ya siku tatu iliyowakutanisha wanahabari na watafiti wa kilimo kutoka nchi tano za Afrika Uganda, Kenya, Burknafaso, Ethiopia na Tanzania ambayo ilikuwa mwenyeji wa semina hiyo iliyoanza juzi jijini Mwanza.



Na Dotto Mwaibale, Mwanza

NCHI za Afrika zimetakiwa kuwekeza kwenye kilimo kwa kuwa kilimo ni biashara na chakula. Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Jukwaa la Bioteknojia kutoka nchini Uganda, Philip Chemonges jijini Mwanza jana wakati akitoa mada kwenye semina ya siku tatu iliyowakutanisha wanahabari na watafiti wa kilimo kutoka nchi tano za Afrika Uganda, Kenya, Burknafaso, Ethiopia na Tanzania ambayo ilikuwa mwenyeji wa semina hiyo.

"Hivi sasa kilimo ni muhimu hivyo ni vizuri nchi za Afrika ziamke na kuwekeza katika kilimo kwani kilimo ni biashara na kinatukomboa kwa chakula" alisema Chemonges. Katika hatua nyingine Meneja wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB), Daniel Otunge amewataka waandishi kutoka nchi hizo kushirikiana na wataalamu wa kilimo ili kupata fursa ya kuandika habari za kilimo kwa ufasaha pasipo kuwepo upotoshaji.

Otunge alisema lengo la semina hiyo iliyoandaliwa na Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo kwa ajili ya Manufaa ya Wakulima Wadogo (AATF) ni kuwakutanisha waandishi wa habari na wataalamu wa kilimo waweze kukutana na kupeana uzoefu wa jinsi ya kuandika habari za kilimo cha Bioteknolojia kwa ufanisi.


MWENGE WA UHURU KUWASILI WILAYA YA UBUNGO KESHO 31/05/2017

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kibamba Chama-Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na Waandishi wa habari

Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 utawasili kesho Tarehe 31 Mei 2017 katika Wilaya ya Ubungo kuanzia saa moja kamili asubuhi na kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo.   
     
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amesema kuwa katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Mradi mmoja wa kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la msingi.

Alisema kuwa Miradi mingine itakayozinduliwa ni Mradi wa Ujenzi wa Jengo la kutolea huduma za VVU katika Kituo cha afya Mbezi, Uzinduzi wa madarasa nane katika shule ya Msingi Malambamawili iliyopo Kata ya Msigani, Uzinduzi wa Kituo cha mabasi SIMU 2000 Kata ya Sinza na Uzinduzi wa Zahaanti ya Mburahati.


RC GAMBO AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTOOGOPA KUSTAAFU


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF jijini Arusha juzi ,wakati akifunga mkutano huo ambapo aliwataka wastaafu watarajiwa kujiandaa kustaafu kwa kubuni miradi mbalimbali ya kuongeza kipato hali itakayosaidia wao kujiendeleza kimaisha(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)


Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Eric Shitindi  akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema ni vyema watumishi wakajianda mapema wakiwemo wa umma na sekta binafsi


Mkuu wa mkoa wa arusha Mrisho Gambo amewataka Watumishi katika sekta za umma kuacha dhana ya kuogopa kustaafu kazi pindi wanapofikia muda wa kustaafu badala yake wanatakiwa kujipanga kabla muda haujafika.

Aidha watumishi wanaogopa kustaafu kwa kuwa wanaanza kujiandaa miaka miwili kabla hali ambayo inawapa uoga mkubwa wastaafu watarajiwa. Mrisho Gambo ameyasema hayo jana wakati akifunga mkutano wa mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) uliokuwa ukiendelea jijini Arusha

Gambo alisema kuwa kwa sasa wastaafu wanapata magonjwa ya moyo kwa kuwa hawajajiandaa na kubuni miradi ambayo inaweza kuwaletea vipato kama mishahara yao ilivyokuwa

Alisema maandalizi ni muimu sana kwa wafanyakazi hata kama bado hawajafikia muda wa kustaafu kwani kustaafu sio ajali bali ni kitu ambacho kipo na kimeshawekewa utaratibu na mifuko ya hifadhi jamii hapa nchini pamoja na Serikali.

"Wastaafu wengi wanakufa pindi wanapoacha kazi hiyo sio sawa ni lazima kila mtu ajiandae na abuni njia mojawapo ya kujiongezea kipato kwani hata kama ukijiajiri mwenyewe ni lazima utapata kipato kama kile ulicho kuwa unalipwa kama sehemu ya ujira wako "aliongeza Gambo.


MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI TANGA

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo kwa wakazi wa Jiji la Tanga kwenye banda lao lililopo katika eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara ya kimataifa


Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiptia kwenye banda la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) wakati alipofungua maonyesho ya kimataifa ya biashara ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga

Monday, May 29, 2017

UMISSETA MKOA WA DAR ES SALAAM YAPAMBA MOTO

Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno akizungumza wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasalimu wanamichezo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Maandalizi ya ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam Kwa Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania yamezidi kupamba Moto katika Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es salaam.

Maandalizi hayo kwa ngazi ya Mkoa kwa ajili ya kupata timu ya Mkoa Wa Dar es salaam yameanza Leo Mei 28, 2017 Kwa kuhusisha Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam ikiwemo Manispaa ya Ilala, Temeke, Kinondoni, Kgamboni na Ubungo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo Kwa ngazi ya Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam Kaimu Katibu Tawala katika upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno amewasihi washiriki kutumia weledi wao wa mafunzo waliyoyapata kuhusu michezo na kuonyesha umahiri wao ili kuchaguliwa katika timu ya Mkoa.


MD KAYOMBO ASHAURI WATANZANIA KUFUATA FURSA ZILIPO

PICHANI: Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuzifuata fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kukuza uchumi wa viwanda.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza wakati akitoa taarifa ya mbio za Mwenge unaotaraji kuzuru katika Manispaa ya Ubungo Tarehe 31, Mei 2017.

Alisema kuwa katika mikoa mbalimbali Mwenge wa Uhuru ulipopita umekutana na fursa ambazo Watanzania wakizitafuta na kuzifanyia kazi wataondokana na uvivu, kukaa bila kufanya kazi na umasikini kwa kuwa sasa Serikali iliyopo madarakani ni ya kazi.

Aliongeza kuwa, nchi nyingi zimekuwa kiuchumi kupitia viwanda na kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda, wananchi wanapaswa kuzichangamkia fursa mbalimbali ili kufanikisha dhamira ya Serikali kufikia uchumi wa viwanda.

MD amesema kuwa Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Ubungo utapita katika Miradi mitano ya Maendeleo ambapo Miradi minne kati ya hiyo itazinduliwa na Mradi mmoja wa Ujenzo wa Kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la Msingi.

Alisema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu jumla ya shilingi Bilioni 2,854,647,991.89

Imetolewa Na;
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo


“MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI BANDARI YA TANGA WAIVA”

Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia akimueleza jambo Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kushoto wakati alipofungua maonyesho ya tano ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.

Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale akizungumza na waandishi wa habari leo

MRADI wa Bomba la Mafuta Mkoani Tanga umefikia kwenye hatua ya wataalamu kukagua njia itakayopitisha miundombinu ya bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Hatua hiyo imekuja baada ya serikali ya Tanzania na Uganda kutiliana saini ya mkataba baina ya nchi na nchi (Iga) kukamilika.

Hayo yalisemwa leo na Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.

Saturday, May 27, 2017

ZINGATIA HAYA UNAPOTAKA KUENDESHA GARI UMBALI MREFU



Na Jumia Travel Tanzania

Linaweza kuwa si jambo la kushangaza kuwaona watu wakisafiri kwenye usafiri wao binafsi kuelekea mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Na hii ni kutokana na maendeleo na mabadiliko ya kiuchumi miongoni mwa watanzania wengi ambapo hapo awali walikuwa wanategemea usafiri wa umma.

Sababu za kusafiri zinaweza kuwa nyingi kama vile kifamilia, kutembelea ndugu na jamaa au vivutio mbalimbali vya kitalii. Lakini je ni wangapi wanayafahamu mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuingia barabarani na usafiri binafsi kwenda umbali mrefu? Jumia Travel imekukusanyia masuala muhimu ambayo usipokuwa makini kuyafuata basi safari yako itakuwa ni shubiri badala ya asali huko njiani.

Jipange kwa safari nzima. Sidhani kama kuna jambo ambalo unaweza kufanikiwa bila ya kujipanga. Vivyo hivyo unapotaka kusafiri ni lazima uweke mipango madhubuti tangu mwanzo mpaka mwisho wa safari yako. Kwa mfano, safari itachukua muda gani, hoteli gani mtafikia, gari utakalolitumia litawatosha watu wangapi, gari litahitaji mafuta kiasi gani mpaka kumaliza safari, nini cha kufanya inapotokea dharura na kadhalika.

Chunguza usafiri wako. Barabarani kuna mengi yanatokea ingawa kuna mengi unaweza kuyadhibiti endapo utachukua tahadhari kabla. Kwa mfano suala la gari kuharibika njiani linaweza kuepukika endapo utachukua muda wako kulipeleka kwa fundi kufanyiwa uchunguzi na matengezo pale yatakapohitajika. Huwezi jua inawezekana injini isingeweza kukupeleka hata nusu ya safari yako au jaribu kuvuta picha gari linapokuharibikia katikati ya msitu wenye wanyama wakali bila ya msaada.

JUMIA TRAVEL YAZINDUA RIPOTI YA UTALII BARANI AFRIKA

KUZIDI kuongezeka kwa watumiaji wa intaneti barani Afrika na kufikia zaidi ya milioni 300 ambayo kiuwiano kwa ueneaji wake ni sawa na 27.7% ni ishara nzuri kwa uchocheaji wa ukuaji wa shughuli za utalii kwa njia ya mtandao.

Hayo yalibainishwa kupitia ‘Ripoti ya Utalii Afrika kwa mwaka 2017’ iliyowasilishwa na Jumia Travel inayojihusisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao, ambapo inaelezea kuwa teknolojia na huduma za simu zimeliingizia bara la Afrika mapato ya ndani kwa 6.7% kwa mwaka 2015 (ambazo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 150 kwa thamani ya kiuchumi), na yanatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 210 (7.6% ya jumla ya pato la ndani la taifa) kufikia mwaka 2020.


LAPF PENSION YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI

Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe akifafanua jambo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo wakati alipkuwa akizungumza katika mkutano wa siku moja na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habaru uliofanyika leo kwenye jengo la Milenium Tower lililopo Makumbusho jijini Dar es salaam mkutano huo wa siku moja umejadili mambo mbalimbali yanayofanywa na mfuko huo kuhusu mafao yanayotolewa kwa wanachama wake lakini pia kutatua changamoto kadhaa zinazokabili mfuko huo Kulia ni Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri TEF Bw. Neville Meena na katikati ni Mwenyeekiti wa TEF Bw. Theophil Makunga.

Kulia ni Ramadhan Mkeyenge Meneja Mafao LAPF na Elia Shola Afisa Mwandamizi Uwekezaji wakiwa katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika mkutano huo leo.


UCHELEWESHAJI PEMBEJEO WAPOROMOSHA KILIMO CHA PAMBA MKOANI GEITA


Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe, (kulia), Elias Kayandabila, akizungumza na waandishi wa habari, walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani Geita kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.

Na Dotto Mwaibale, Mbogwe

KUCHELEWA kufikishwa kwa pembejeo za kilimo kwa wakati kwa wakulima wa pamba imeelezwa kuwa kunachangia kuporomosha kilimo hicho wilayani Mbogwe mkoani Geita.

PICHANI KULIA: Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi akizungumza na ujumbe huo.


Hayo yalielezwa wilayani humo jana na Magua Mayala, mkulima wa pamba wa Kitongoji cha Kakumbi Kata ya Lugunga wilayani Mbogwe mkoani Geita wakati akizungumza na waandishi wa habari walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani humo kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.

Mayala alisema changamoto kubwa waliyonayo wakulima katika wilaya hiyo ni kucheleweshewa pembejeo hali inayowafanya waende kutafuta mbegu ambazo hazina ubora ambazo zinawasababishia wakulima kupata mavuno kidogo ukilinganisha na maeneo ambayo wanapata mbegu bora.

"Tunaiomba serikali itusaidie kutufikishia pembejeo za kilimo kwa wakati ili kuliinua zao la pamba ambalo ni la biashara katika wilaya yetu" alisema Mayala.

Alisema alipanda ekari moja ya pamba kwa kutumia mbegu duni ambapo alipata kilo 100 alizouza sh. 200,000 na kueleza kuwa changamoto kubwa ni pamoja na dawa za kuulia wadudu waharibifu wa pamba na hata wakipata dawa hizo haziui wadudu.


MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA ATOA CHETI KWA MTUNZA MALI ZA UMMA


Na Leonce Zimbandu

MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela ametoa cheti cha shukurani kwa Mkazi wa Mtaa wa Kichangani kata ya Majohe, Gabriel Macheho (pichani) baada ya kutambua mchango wake wakuhifadhi na kutunza rasilimali za umma.

Moja ya rasilimali hizo ni pamoja na kusimamia eneo la umma lisichukuliwe na kumilikiwa na watubinafsi, likiwamo eneo lamachimboyamchangalililokuwalikimilikiwanaMbezi Tile.

Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo, Tabu Shaibu alimkabidhi Macheho cheti hivi karibuni kwa niaba ya Mkurugenzi ili kutoa motisha kwa wananchi wenye moyo wakutoa utetezi wa mali za umma.

Alisema Manispaa imeamua kutoa cheti hicho baada ya kutambua mchango aliotoa mkazi huyo kwa kufuatilia hadi kufanikiwa kupatikana kwa eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii, ikiwamo ujenzi wa soko na shule.

“ Tunapaswa kuonesha uzalendo wakufuatilia mambo yenye manufaa kwa jamii ilikuishaidia jamii inayo kuzunguka,” alisema.

Mkazi wa Majohe Andrew Msuya alisema amefurahishwa na kitendo cha Serikali kutambua mchango wa wananchiwachini, hiyo italeta chachu kwa watu wengine kuendeleza na kuhifadhi mazingira.

WAZIRI MWIJAGE MGENI RASMI MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA TANGA


Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuwa mgeni kwenye maonyesho ya kimataifa yatakayoanza kesho kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga


Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa kwenye na Waziri Mwijage

Friday, May 26, 2017

JE WEWE UNA MLEVI WA MAJI? SOMA HII INAKUHUSU

-->Wataalam wanashsuri unywaji maji mengi, lakini ukweli ni kwamba yaweza kuwa hatari kubwa…
- Yadaiwa maji huongeza uwezo wa kufikiri na kupunguza maumivu ya kichwa
- Wataalamu wanahoji athari za kunywa maji kupindukia
- Wanashauri unywaji wa lita moja mpaka mbili ni hatari
- Hivyo ni kwa kiasi gani tunatakiwa kunywa maji kwa siku?


Na Mwandishi Wetu (kwa msaada wa mitandao ya internet)

Unywaji maji wa bilauri sita mpaka nane kwa siku, kama ambayvo tumekuwa tukiambiwa inaongeza uwezo wa kufikiri, ngozi na nguvu zaidi, huondoa maumivu ya kichwa na kusaidia kuondoa sumu mwilini na hata kuongeza hamu ya kula chakula.

Wataalamu wameanza kuchunguza kama unywaji maji mengi una faida kiafya, na kushauri kuwa ni hatari kunywa maji kupita kiwango kinachoshauriwa cha lita moja na nusu mpaka mbili kwa siku. Wengine wamekwenda mbali zaidi kutaadharisha kuwa mahaba yetu na maji mengi yanaathari kubwa kiasi cha kuweka afya zetu hatarini.

Miaka michache iliyopita watu wengi wameripoti kuwa walevi (addicted) wa maji sababu tu ya matamanio ya kuwa na ngozi nzuri, kuondoa sumu mwilini na kuwa na nguvu, lakini matokeo yake wameshindwa kuishi bila maji na kuwa na wasiwasi kuwa hawawezi kuishi hata muda mfupi bila maji.


CCM YAMPONGEZA JPM SAKATA LA MCHANGA WA MADINI, YALAANI VIKALI MAUAJI MKOANI PWANI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam. Picha Zote na Mathias Canal


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kutekeleza sera na kuisimamia ilani ya ushindi ya CCM ya mwaka 2015/2020 na kuwaomba watanzania wote kwa kauli moja pasina itikadi za vyama kumuunga mkono kwani atakuwa imara na madhubuti zaidi katika utendaji wake iwapo ataungwa mkono na watanzania wote.

Chama cha Mapinduzi (CCM) Kimetoa pongezi hizo kutokana na maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli mara baada ya kupokea Ripoti ya kamati iliyokuwa inachunguza Hatma ya mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Magufuli Machi 29 mwaka huu ikiwajumuisha Profesa Abdulkarim Hamisi Mruma (Mwenyekiti), Profesa Justiania Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dokta Yusuph Ngenya, Dokta Joseph Yoweza Phili, Dokta Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.


Thursday, May 25, 2017

NEW MUSIC VIDEO: LAVALAVA - TUACHANE (OFFICIAL MUSIC VIDEO)




MBEGU BORA ZA MUHOGO ZINAHITAJIKA KUNUSURU WAKULIMA WILAYANI CHATO

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ipandikilo kilichopo katika Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Lazaro Kagundulilo (kulia), akizungumza na wanahabari pamoja na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) na , Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB), wilayani humo jana. Wataalamu hao wa kilimo wapo katika wilaya hiyo kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa Mkoa wa Geita.


Maofisa ugani wakiangalia eneo ambalo patalimwa shamba dogo la mfano katika Kijiji cha Kibehe Kata ya Kigongo.

Na Dotto Mwaibale, Chato

 MBEGU bora za zao la mhogo zinazositahimili magonjwa ya Batobato na michirizi kahawia zinahitajika ili kuweza kunusuru kukumbwa na baa la njaa kwa wakulima wa zao hilo katika Wilaya ya Chato mkoani Geita baada ya mbegu walizolima msimu huu kushambuliwa na magonjwa.

Wananchi wa wilaya hiyo wanategemea zaidi zao la mhogo kama chakula chao kikuu pamoja na biashara lakini hivi sasa hali siyo shwari kutokana na mihogo waliyopanda kushambuliwa na magonjwa.

Akizungumza na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na watafiti wa kilimo kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), walio katika ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija wilayani humo leo, mkulima wa zao la mhogo katika Kijiji cha Ipandikilo, Andrew Misano alisema changamoto kubwa waliyonayo ni magonjwa yanayoshambulia zao hilo.

Misano alisema msimu wa mwaka huu umekuwa tofauti na misimu mingine kutokana na zao la mhongo kushambuliwa na magonjwa ya batobato na michilizi kahawia. "Msimu huu nimelima ekari saba za mhogo lakini sitegemei kuvuna chochote kutokana na kushambuliwa na magonjwa hayo" alisema Misano.


Wednesday, May 24, 2017

MELANIA TRUMP HATAKI KABISA KUMSHIKA MUMEWE MKONO?

PICHANI: Mke wa Rais wa Marekani, Melania baada ya kukwepa mkono wa mumewe, baada ya kuwasili jijini Rome wakati wanashuka katika ndege ya Rais, Air Force One jumanne jioni katika Uwanja wa Kimataifa wa Vinci-Fiumicino. Picha-Getty Image


Na Mwandishi Wetu, Rome

Ndoa ya Donald na mkewe Melania Trump imekuwa ikifuatiliwa kwa muda sasa jambo linaloashiria kuwa haiku shwari, ikiwa ni siku ya pili Melania alipokataa kumshika mkono mumewe kitendo ambacho kimepokelewa kwa hisia tofauti.

Siku ya Jumanne, wawili hao baada ya kuwasili Rome, Italy ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku tisa ya kueneza ‘amani duniani’ ziara iliyohusisha nchi za Saudi Arabia, Israel na kuishia Italy, ambapo wawili hao watakutana na Papa Francis, Vatican na kutembelea makazi ya Papa katika kanisa kongwe la Sistine Chapel.
Video ikonesha tendo hilo wakati wanashuka kwenye ndege jumanne

Wakiwa wanajiandaa kushuka katika dege la Rais, Air Force One, katika Uwanja wa Kimataifa wa Vinci-Fiumicino, Rais alijaribu kumshika mkewe mkono lakini bila mafanikio Melania aliinua mkono kurekebisha nywele zake zilipozokuwa zinapeperushwa na upepo. Mkono wa Rais ulibaki hewani kabla hajaamua kumshika kwa nyuma mgongoni.

Tukio hilo ni mwendelezo wa tukio la jumatatu (siku moja kabla) halijapotea ambapo Melania alionekana akipotezea mkono wa mumewe walipokuwa wakifuatana baada tu ya kutua nchini Israel.


RASTAMAN MZEE WA MIAKA 110, BADO ANA NGUVU NA ANAIMBA MSIKILIZE HAPA

Rasta mzee anayedaiwa kuwa na miaka 110, akiimba nyimbo 'By the rivers of Babylon' Msikilize hapa chini



WANACHATO CHANGAMKIENI KILIMO CHA MIHOGO KINA TIJA KATIKA SOKO LA KIMATAIFA


Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akizungumza na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) pamoja na wanahabari walipofika ofisini kwake wakiwa katika ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa mkoa huo leo.



Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba kabla ya kuanza ziara ya mafunzo hayo.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akiwaonesha shamba la mfano la mahindi ambalo lipo nje ya ofisi yake wataalamu hao wa kilimo pamoja na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange na kushoto ni Mratibu wa Jukwaa hilo Tanzania, Philbert Nyinondi.

Na Dotto Mwaibale, Chato

MAOFISA Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita wameombwa kuwa weredi zaidi katika masuala ya kilimo ili elimu waliyonayo waweze kuitoa kwa wakulima ili nao waweze kulima kilimo chenye tija cha zao la mihogo ili zao hilo liweze kukubalika katika soko la kimataifa.

Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon wakati akitoa mafunzo kwa maofisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita leo ambayo yameandaliwa na Tume ya Sayansi ya Teknolojia (Costech) kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB).

Alisema hivi sasa nchi ya China na Tanzania zimesaini mkataba wa ununuzi wa zao la muhogo jambo ambalo ni fursa kwa wakulima wetu wa hapa nchini wakiwemo wa kutoka wilaya ya Chato. "Hii ni fursa kubwa kiuchumi lakini ni vema sasa tukaingia katika kilimo chenye tija ili mihogo yetu iweze kuingia katika soko la kimataifa badala ya kuendelea na kilimo kisicho na tija" alisema Simon.


SBL YATOA ZAWADI YA GARI AINA YA SHS 50M/- KWA MSAMBAZAJI BORA


Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo (wa kwanza kushoto) akimkabidhi nyaraka za gari aina ya Heicher lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika, ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka huu wa fedha 2017.wanaoshuhudia katikati ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy ,na Baraka Kilimba Meneja Mauzo Baraka Kilimba na mwishoni ni Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha


Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo Akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu zawadi ya msambazaji bora ambapo MM Group kutoka Mpanda aliibuka mshindi ,kulia kwake ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy na kushoto kwake ni Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika,mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.


Dar es Salaam, Mei 24, 2017

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetoa zawadi ya gari aina ya Heicher lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa MM Group, ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka huu wa fedha 2017.

Kampuni ya MM Group ambayo ina makao yake wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi iliwashinda wasambazaji wengine 85 walioshiriki kwa ajili ya kupata zawadi hiyo ya kipekee.

Akiendesha hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya SBL Temeke, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo alimpongeza mshindi huku akithibitisha kujikita kwa kampuni hiyo ya bia katika kutambua juhudi zinazofanywa na wateja wake katika kuunga mkono ukuaji kwa kampuni.


BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AMTUMBUA WAZIRI PROF MUHONGO




Tuesday, May 23, 2017

MAFUTA YA NAZI YANAUA ZAIDI YA ASILIMA 93 YA SELI ZA SARATANI YA TUMBO

-->
Na Mwandishi Wetu (kwa msaada wa mitandao)

Katika utafiti uliofanywa mwaka 2014 na kuchapisha kuwa tindikali aina ya lauric (ambayo ni asilimia 50 ya katika mafuta ya nazi) inauwezo wa kuua asilimia 93 ya seli zinazosababisha saratani ya tumbo katika mwili wa binadamu baada ya saa 48 za matibabu.

Chakushangaza ni kwamba tindikali ya Lauric ni sumu kwa seli za saratani sababu ni chanzo cha kemikali inayoshambulia seli za saratani na kupunguza uwezo wa kuishi jambo ambalo seli za saratani huitaji kujilinda katika kujihakikishia uhai wake.

Taarifa iliyoko kwenye chapisho la mwaka 2014, februari 26, katika mtandao wa Complete Health and Happiness, imeeleza kuwa wakati wanasayansi wanavumbua uwezo mkubwa wa mafuta ya nazi katika mapambano dhidi ya saratani, umuhimu wa mafuta ya nazi kiafya kwa binadamu yamekuwa yakitangazwa kufahamika kupitia tafiti mbalimbali za wataalamu.

Mafuta ya nazi yanaua virusi mbalimbali, bakteria, fangas na vijidudu. Yanasaidia mfumo wa usagaji chakula pamoja na metaboliki ya ini, hupunguza maumivu na kurutubisha ngozi pamoja na kutibu majeraha haraka.


MAOFISA UGANI WATAKIWA KUWA NA MASHAMBA YA MFANO


Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo.

Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Stella Chirimi akitoa mada katika mafunzo hayo.


Na Dotto Mwaibale

MAOFISA Ugani wametakiwa kuwa na mashamba ya mfano ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza masuala ya kilimo kutoka kwao.

Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru, Stellah Chirimi wakati akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB).

"Ni vema kila ofisa ugani akawa na shamba la mfano ambalo litasaidia wakulima kwenda kwao kujifunza kilimo bora badala ya kuwaacha bila ya kuwasaidia kupitia mashamba hayo ya mfano.

Katika hatua nyingine Chirimi alisema uzalishaji wa zao la pamba umeshuka kutokana na maofisa kilimo kushindwa kuwafikia wakulima kwa ajili ya kuwapa elimu ya kilimo bora na cha kisasa.

Alisema kuna kila sababu ya kutolewa elimu kwa wakulima kuhusu mbegu bora ya pamba ambayo ikitumika itaongeza tija katika uzalishaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini.

Monday, May 22, 2017

JE MAZIWA YA MAMA YANAWEZA KUTIBU SARATANI?

- Wanasayansi wabahatisha uvumbuzi wa tiba mpya ya saratani yatokanayo na maziwa ya mama

Na Mwandishi Wetu (kwa msaada wa mitandao)

Faida ya maziwa ya mama imekuwa ikielezwa kwa muda mrefu sana, lakini wataalamu wameanza kujaribu uwezekano wa maziwa hayo katika tiba ya saratani.

Uvumbuzi wa bahati mbaya wa matokeo ya vimea vilivyomo katika maziwa ya mama vilivyopewa jina “Hamlet”na wanasansi, ikimaanisha ‘yenye nguvu na uwezo wa kupambana na seli hatari zinazosababisha uvimbe wa saratani’

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Lunt, Sweeden wameeleza uwezekano chanya baada ya kuchunguza uwezo mkubwa wa Hamlet kwa wagonjwa wenye saratani ya kibofu.  Katika majaribio ya awali, waliochomwa sindano yenye Hamlet uvimbe ulianza kupungua na wengine kuisha baada ya kupimwa kupitia njia ya mkojo siku chache baadae.

“Kuna jambo la ajabu kuhusu uwezo wa Hamlet kwenda kushambulia uvimbe na kuteketeza kabisa” alisema Dr. Catharina Svanborg akiliambia gazeti la Daily Mail. Lakini uvumbuzi huo ulipatikana kwa bahati mbaya wakati wakichunguza kuhusu dawa ya antibiotics.


MBUNGE LUSHOTO AWAPA POLE WAKULIMA WA MBOGAMBOGA, AWATAKA KUONGEZA UZALISHAJI


Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mkoani Tanga (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia kulia akitazama namna mbogamboga za wakulima kwenye Jimbo lake zilivyoharibika hivi karibuni kutokana na miundombinu ya barabara ya Mombo hadi Lushoto kudondokewa na vifusi na mawe kabla ya kuondolewa na wakala wa barabara mkoani Tanga (Tana Road ) ambapo aliwapa pole wakulima na kuwataka kuongeza uzalishaji


Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mkoani Tanga (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katika akizungumza na wakulima wa mbogamboga kwenye Jimbo lake hivi karibuni ambao bidhaa zao ziliharibika kutokana na miundombinu ya barabara ya Mombo hadi Lushoto kudondokewa na vifusi na mawe kabla ya kuondolewa na wakala wa barabara mkoani Tanga (Tana Road ) ambapo aliwapa pole wakulima na kuwataka kuongeza uzalishaji

MKUU WA WILAYA YA UBUNGO ATOA MAAGIZO MANNE KUTEKELEZWA, IKIWEMO KUJENGWA KWA MADARASA NANE SHULE YA MSINGI UBUNGO PLAZA


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza katika Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 19, 2017 ameagiza kujengwa madarasa nane mapya katika shule ya Msingi Ubungo Plaza Jijini Dar es salaam kutokana Na uchakavu wa Majengo ya madarasa yaliyopo sasa.

Ametoa agizo hilo katika mkutano wake na uongozi wa shule hiyo ukiwajumuisha mtendaji na wajumbe wa mitaa,walimu na wananchi  ambao waliohudhuriwa katika viwanja vya  shule ya Msingi Ubungo Plaza.

Mhe Makori amesema kuwa ili kuboresha elimu katika Wilaya ya Ubungo ni wazi kuwa ni lazima kuwe Na miundombinu rafiki kwa wanafunzi wanapokuwa darasani kwa ajili ya masomo kwani ubovu wa Majengo ya shule,ubovu na uhaba wa vyoo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea wanafunzi kufeli kutokana na kutokuwa Na miundombinu rafiki.


HATUA ZA KUFUATA BAADA YA KUACHWA NA NDEGE



Na Jumia Travel Tanzania

Ni jambo la kawaida kuachwa na usafiri kama vile basi, boti, treni au ndege licha ya kufanya maandalizi ya kutosha. Baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia mtu mpaka kuachwa na usafiri ni kama vile foleni barabarani, ajali au usafiri kupata matatizo na kukosea muda wa kuwasili.

Hali ya kuachwa na usafiri ni ngumu sana kama haijawahi kukutokea kabla na hauna mbinu mbadala ya kukuwezesha kusafiri kama ulivyokukusudia. Zipo hatua kadhaa za kufuata pindi uchelewapo ndege ambazo Jumia Travel ingependa uzifahamu na kuzizingatia pindi utakapokumbwa na changamoto kama hii.

Wasiliana na shirika la ndege unalosafiri mara moja. Kitu cha kwanza kabisa baada ya kugundua kwamba utachelewa au umechelewa ndege ambayo ulitakiwa kusafiri nayo ni kuwasiliana na shirika husika. Mara nyingi mawasiliano huwemo kwenye tiketi au tovuti ya shirika. Kwa kufanya hivyo utajua ni msaada gani wanaweza kukupatia kulingana na hali uliyopo.

Kuwa makini na sheria na masharti ya tiketi uliyokata. Kila shirika la ndege linakuwa na taratibu za uendeshaji wa safari zake. Zipo ambazo zinawasafirisha na ndege nyingine wateja wao waliochelewa, zingine siku inayofuata kama hamna kwa siku hiyo na zingine kutoza malipo ya ziada kwa kuchelewa ndege. Kwa hiyo kabla ya kukata tiketi ulizia taarifa hizo au soma kwenye tiketi yako kama zipo.

Usihamaki/usiwe na hofu. Wewe sio wa kwanza kuachwa na ndege hali hiyo ishawakuta watu wengi hivyo vuta pumzi na tuliza akili yako ili ujue nini cha kufanya. Usipohamaki utaweza kupata suluhu ya tatizo haraka sana kama vile kuulizia cha kufanya, kuahirisha au kutafuta uwanja wa ndege ulio karibu ili usafiri na kuwahi shughuli zako kama ulivyopanga. Kwani kama kuchelewa umekwisha chelewa hakuna cha kufanya kutokana na hali hiyo.

Sunday, May 21, 2017

MKUTANO WA 18 WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI DAR ES SALAAM


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kwenye Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimtambukilisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Rwanda Mhe. Francois Kanimba kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Mhe. Gaston Sindimwo kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam


Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kikanda Dkt. Augustine Mahiga