Wednesday, May 24, 2017

MELANIA TRUMP HATAKI KABISA KUMSHIKA MUMEWE MKONO?

PICHANI: Mke wa Rais wa Marekani, Melania baada ya kukwepa mkono wa mumewe, baada ya kuwasili jijini Rome wakati wanashuka katika ndege ya Rais, Air Force One jumanne jioni katika Uwanja wa Kimataifa wa Vinci-Fiumicino. Picha-Getty Image


Na Mwandishi Wetu, Rome

Ndoa ya Donald na mkewe Melania Trump imekuwa ikifuatiliwa kwa muda sasa jambo linaloashiria kuwa haiku shwari, ikiwa ni siku ya pili Melania alipokataa kumshika mkono mumewe kitendo ambacho kimepokelewa kwa hisia tofauti.

Siku ya Jumanne, wawili hao baada ya kuwasili Rome, Italy ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku tisa ya kueneza ‘amani duniani’ ziara iliyohusisha nchi za Saudi Arabia, Israel na kuishia Italy, ambapo wawili hao watakutana na Papa Francis, Vatican na kutembelea makazi ya Papa katika kanisa kongwe la Sistine Chapel.
Video ikonesha tendo hilo wakati wanashuka kwenye ndege jumanne

Wakiwa wanajiandaa kushuka katika dege la Rais, Air Force One, katika Uwanja wa Kimataifa wa Vinci-Fiumicino, Rais alijaribu kumshika mkewe mkono lakini bila mafanikio Melania aliinua mkono kurekebisha nywele zake zilipozokuwa zinapeperushwa na upepo. Mkono wa Rais ulibaki hewani kabla hajaamua kumshika kwa nyuma mgongoni.

Tukio hilo ni mwendelezo wa tukio la jumatatu (siku moja kabla) halijapotea ambapo Melania alionekana akipotezea mkono wa mumewe walipokuwa wakifuatana baada tu ya kutua nchini Israel.


“Inaelekea kuna shida katika ndoa yao, toka Donald Trump alipoapishwa kuwa Rais wa Marekani, tunachoona hapa ni kwamba Melania hataki kuwa karibu na mumewe” alieleza mtaalam wa lugha ya vitendo (Body Language) ambaye ni mfanyakazi wa idara ya ulinzi nchini Marekani, Susan Constantine.

Haya si mambo binafsi tena, Melania anajua kuwa kamera zinafuatilia kila kinachoendelea, ni kama anampa ujumbe wa aina fulani hivi mumewe kuwa hawezi kuendelea kujificha katika ngozi ya kondoo.

Kitendo cha Melania kuinua mkono kinaashiria uvunjifu wa heshma haswa pale ambapo Rais amebaki mkono unasubiri na mwishowe kumshika nyuma ili kumwongoza kwenye ngazi wakati wanashuka ngazi.

Hata hivyo ukiangalia umbali kati yao, kila mmoja angeweza kushuka ngazi mwenyewe kwa maana kwamba kuna nafasi kubwa sana kati yao jambo ambalo linaashiria kuwa kuna utengano baina yao, aliongeza mtaalamu huyo

“Kwa kutengeneza nywele zake kwa kutumia mkono uliokuwa karibu na mumewe, ni wazi Melania hakutaka kushikwa mkono na mumewe, kwani aliona mkono wa mumewe akitaka kumshika” aliongeza Susan.

Shida ilianza kuonekana siku ya kwanza baada ya Donald kuapishwa wakiwa wafungua muziki kwa mara ya kwanza kama mke na mume katika nafasi ya Rais wa taifa la Marekani, n ahata siku walipokwenda White House na kupokelewa na watangulizi wao Baraka na Michelle Obama, jambo ambalo watu wengi walilitafsiri kama kitendo kisichokuwa cha kawaida.

Chini ni video inayoonesha Melania akipiga mkono wa mumewe baada ya kuwasili nchini Israel Jumatatu




No comments:

Post a Comment