Akifanya mahojiano yake ya kwanza mara baada ya kuachiwa kutoka gerezani kwa kuhusishwa na kifo cha nguli wa muziki wa pop duniani marehemu Michael Jackson, aliyekuwa daktari wake Conrad Murray(Kulia) alieleza kuwa muimbaji huyo nyota hakuwahi kupata mtoto hata mmoja kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa.
Katika mahojiano maalumu na gazeti la The Daily Mail la nchini Uingereza hivi karibuni daktari huyo alikaririwa akisema, alikuwa anaushikilia uume wa Michael Jackson kutokana na matatizo ya kiafya ambayo yalikuwa yanamsumbua kila usiku.
Alidai kuwa marehemu Michael Jackson hakuwa baba wa hata mtoto wake mmoja, aliathiriwa na dawa kiasi cha kufikia hatua ya kuhitajika kuwa anavaa condom ili kuuzuia mkojo uliokuwa unatoka wenyewe kwenye uume wake.
"Unataka kujua ni namna gani ambavyo tulikuwa na ushirikiano wa karibu naye (Michael Jackson)?" Nilikuwa nashikilia uume wake kila usiku ili kuuweka sawa kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na kifafa alikuwa hajiwezi usiku, alikaririwa Daktari huyo akisema.
Daktari huyo alienda mbali zaidi akadai kuwa, Michael Jackson alikuwa anapenda kuvaa suruali nyeusi kila siku ili iweze kumsaidia kuhifadhi aibu zake.
Aliweka wazi kuwa Michael alikuwa anapenda kuvaa suruali nyeusi kila siku kwa sababu uume wake ulikuwa unadondosha maji maji kila saa.
Kutokana na hali hiyo alikuwa analazimika kuvaa condom kila siku na ilikuwa ni shida kwake kwa kutofahamu jinsi ya kuvaa hali iliyokuwa inampelekea daktari huyo kulazimika kumvalisha kila siku.
Hata hivyo, Daktari huyo alisema anaamini kifo cha Michael Jackson ambacho kilitokea hivi karibuni kilisababishwa na yeye (Michael)mwenyewe kutokana na kujidunga sindano ambapo aliweza kujiridhisha baada ya kuingia chumbani kwake siku ya kifo.
Pia alisema, watoto watatu ambao wanadaiwa ni wa Michael Jackson wana baba tofauti na anaamini nyota huyo hakuwa na chake hapo kwa kuwa aliwahi kumtamkia kuwa mwanadada Debbie Rowe hajawahi kulala naye.
"Michael aliwahi kunieleza kuwa, kamwe hajawahi kulala na Debbie Rowe," alikaririwa akisema.
No comments:
Post a Comment