Kampuni hiyo sasa inawawezesha wateja wa Airtel kote nchini kutoa mpaka kiasi cha shilingi milioni 3 kwa wateja waliosajili laini zao kikamilifu kwa kila siku anapotaka kutoa pesa kwa siku.
Vilevile wateja hao wanaweza kuweka mpaka kiwango cha shilingi Milioni 5 kwa siku.
Akiongea wakati wa kutangaza ongezeko hilo, Meneja wa Airtel Money Asupya Nalingingwa (pichani) alisema kwa sasa wateja watakuwa na uwezo wa kutoa na kuweka kiasi kikubwa cha fedha na kuepuka usumbufu wa kutoa au kuweka pesa mara nyingi.
“Wateja wa Airtel Money na wateja wote wa simu za mkononi wataweza kunufaika kwa kiasi kikubwa. Wataepuka usumbufu na kujihakikishia usalama wakutosafiri na pesa nyingi kwa kuwa Airtel Money inaliwezesha hilo ambapo kwa sasa watatoa na kuweka kiasi kikubwa cha fedha tofauti na ilivyokuwa awali,” alisema Bw, Nalingigwa.
Aliongeza kwa kusema wateja wa Airtel Money ambao wameweshwa kwa muda mrefu kutuma na kupokea pesa bure kupitia huduma ya ‘Hakatwi Mtu hapa’ wanapata faida kwa kuokoa kiasi cha shilingi elfu 20 kila wanapotuma Milioni 3 Tzs na hivyo inasaidia kupunguza makali ya maisha na kurahisisha shughuli mbalimbali zikiwemo za kibiashara.
“Kama ningekuwa mfanyabiashara au mtu mwingine ambaye natumia pesa kwenye mzunguko kila siku, kupitia ongezeko hili ningejihisi mwenye faraja sana kwani shughuli zangu zingeenda vyema,” alimalizia Bw, Nalingigwa.
Kupitia ongezeko hilo kila mwananchi anaweza kutuma na kuweka kiasi cha fedha kulingana na mahitaji yake katika muda wowote unaomfaa.
No comments:
Post a Comment