Tuesday, May 23, 2017

MAFUTA YA NAZI YANAUA ZAIDI YA ASILIMA 93 YA SELI ZA SARATANI YA TUMBO

-->
Na Mwandishi Wetu (kwa msaada wa mitandao)

Katika utafiti uliofanywa mwaka 2014 na kuchapisha kuwa tindikali aina ya lauric (ambayo ni asilimia 50 ya katika mafuta ya nazi) inauwezo wa kuua asilimia 93 ya seli zinazosababisha saratani ya tumbo katika mwili wa binadamu baada ya saa 48 za matibabu.

Chakushangaza ni kwamba tindikali ya Lauric ni sumu kwa seli za saratani sababu ni chanzo cha kemikali inayoshambulia seli za saratani na kupunguza uwezo wa kuishi jambo ambalo seli za saratani huitaji kujilinda katika kujihakikishia uhai wake.

Taarifa iliyoko kwenye chapisho la mwaka 2014, februari 26, katika mtandao wa Complete Health and Happiness, imeeleza kuwa wakati wanasayansi wanavumbua uwezo mkubwa wa mafuta ya nazi katika mapambano dhidi ya saratani, umuhimu wa mafuta ya nazi kiafya kwa binadamu yamekuwa yakitangazwa kufahamika kupitia tafiti mbalimbali za wataalamu.

Mafuta ya nazi yanaua virusi mbalimbali, bakteria, fangas na vijidudu. Yanasaidia mfumo wa usagaji chakula pamoja na metaboliki ya ini, hupunguza maumivu na kurutubisha ngozi pamoja na kutibu majeraha haraka.


Wataalamu na watafiti wanasema mafuta ya nazi huweza kuwasaidia pia watu wenye tatizo la ugonjwa wa kisukari, kwani inaonesha kusababisha ongezeko la kolestral yenye faida kwa wanawake, ambapo ongezeko hilo husababisha kupungua uzito pamoja na mafuta mafuta yaliyoko tumboni ikifananishwa na mafuta yatokanayo na soya.

Mafuta ya nazi kwa sasa yanatumika katika majaribio ya tiba mbalimbali ikiwemo mafuta mabaya kwa magonjwa ya muda mrefu ya moyo, kupambana na magonjwa ya kupooza, na shinikizo la damu pamoja na kiwango cha sukari mwilini.

Kiwango cha tindikali ya lauric kinachopatikana katika mafuta ya nazi (ambacho ni asilimia 50) ni kiwango kikubwa unachoweza kupata katika nazi ukifananisha chakula kingine chochote.

Cha kufurahisha ni kwamba, tindikali ya Lauric inaweza kupatikana kwa asilimia 2 kwenye maziwa ya ngombe, ikimaanisha kwamba mwanadamu anahitaji vyanzo vingine ili kupata kiwango kikubwa cha tindikali hiyo. Hata hivyo tafiti hizo hazimaanishi kuwa nazi ni dawa ya saratani, bali kuna vyanzo vingi asilia vya kupambana na ugonjwa huo hatari, tafiti zinavyozidi kufanyika ndivyo wataalamu wataweza kushirkishana katika kutafuta tiba ya ugonjwa huo kwa njia ya asili zaidi kuliko kutegemea majibu kutoka kwa watafiti wa dawa za kemikali


No comments:

Post a Comment