Monday, May 22, 2017

JE MAZIWA YA MAMA YANAWEZA KUTIBU SARATANI?

- Wanasayansi wabahatisha uvumbuzi wa tiba mpya ya saratani yatokanayo na maziwa ya mama

Na Mwandishi Wetu (kwa msaada wa mitandao)

Faida ya maziwa ya mama imekuwa ikielezwa kwa muda mrefu sana, lakini wataalamu wameanza kujaribu uwezekano wa maziwa hayo katika tiba ya saratani.

Uvumbuzi wa bahati mbaya wa matokeo ya vimea vilivyomo katika maziwa ya mama vilivyopewa jina “Hamlet”na wanasansi, ikimaanisha ‘yenye nguvu na uwezo wa kupambana na seli hatari zinazosababisha uvimbe wa saratani’

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Lunt, Sweeden wameeleza uwezekano chanya baada ya kuchunguza uwezo mkubwa wa Hamlet kwa wagonjwa wenye saratani ya kibofu.  Katika majaribio ya awali, waliochomwa sindano yenye Hamlet uvimbe ulianza kupungua na wengine kuisha baada ya kupimwa kupitia njia ya mkojo siku chache baadae.

“Kuna jambo la ajabu kuhusu uwezo wa Hamlet kwenda kushambulia uvimbe na kuteketeza kabisa” alisema Dr. Catharina Svanborg akiliambia gazeti la Daily Mail. Lakini uvumbuzi huo ulipatikana kwa bahati mbaya wakati wakichunguza kuhusu dawa ya antibiotics.

“tulikuwa tunatafiti kuhusu vijidudu vya antibiotics huku tukitambua kuwa maziwa ni chanzo kizuri sana cha uwezo huo” alieleza Dr. Svanborg na kuendelea, wakati tunatafiti tulihitaji seli za mwanadamu na bakteria na tukachagua uvimbe wa mwanadamu kwa malengo maalumu”

“kwa mshangao mkubwa, tulipoweka vimelea hivyo vitokanavyo na maziwa ya mama, uvimbe ule ulisinyaa na kufa. Ilitushangaza sana” aliongeza Dr. Svanborg. Watafiti hao wanaamini kuwa kunatokea majibu pale maziwa ya mama yanapokutana na uvimbe. Inatengeneza protini ijulikanayo kama alpha-lactalbumin, inayo lenga seli za saratani.


kimelea hicho kilichopo katika maziwa ya mama, kinalenga seli za saratani pekee, jambo ambalo linasaidia kuleta mbadala wa tiba za mionzi ya chemotherapy na radiotherapy, ambazo madhara yake ni pamoja na afya hata wakati inashambulia seli za saratani.

Wanasayansi wanaamini vimelea hivyo vilivyoko katika maziwa ya mama vinaweza kuwasaidia wagonjwa wa saratani ya tumbo pamoja na shingo ya uzazi. Majaribio ya kimelea cha Hamlet dhidi ya saratani nyingine kwa sasa yanaendelea ili kuona matokeo yake.

No comments:

Post a Comment