Friday, May 26, 2017

JE WEWE UNA MLEVI WA MAJI? SOMA HII INAKUHUSU

-->Wataalam wanashsuri unywaji maji mengi, lakini ukweli ni kwamba yaweza kuwa hatari kubwa…
- Yadaiwa maji huongeza uwezo wa kufikiri na kupunguza maumivu ya kichwa
- Wataalamu wanahoji athari za kunywa maji kupindukia
- Wanashauri unywaji wa lita moja mpaka mbili ni hatari
- Hivyo ni kwa kiasi gani tunatakiwa kunywa maji kwa siku?


Na Mwandishi Wetu (kwa msaada wa mitandao ya internet)

Unywaji maji wa bilauri sita mpaka nane kwa siku, kama ambayvo tumekuwa tukiambiwa inaongeza uwezo wa kufikiri, ngozi na nguvu zaidi, huondoa maumivu ya kichwa na kusaidia kuondoa sumu mwilini na hata kuongeza hamu ya kula chakula.

Wataalamu wameanza kuchunguza kama unywaji maji mengi una faida kiafya, na kushauri kuwa ni hatari kunywa maji kupita kiwango kinachoshauriwa cha lita moja na nusu mpaka mbili kwa siku. Wengine wamekwenda mbali zaidi kutaadharisha kuwa mahaba yetu na maji mengi yanaathari kubwa kiasi cha kuweka afya zetu hatarini.

Miaka michache iliyopita watu wengi wameripoti kuwa walevi (addicted) wa maji sababu tu ya matamanio ya kuwa na ngozi nzuri, kuondoa sumu mwilini na kuwa na nguvu, lakini matokeo yake wameshindwa kuishi bila maji na kuwa na wasiwasi kuwa hawawezi kuishi hata muda mfupi bila maji.

Profesa Mark Whiteley, mtaalamu wa upasuaji misuli na mwanzilishi wa kliniki ya Whiteley, London, Uingereza ni kati ya wataalamu wanaoweka bayana wasiwasi wao juu ya tabia ya unywaji maji kupita kiasi na kwamba baada ya muda hubadilisha kemikali za kwenye ubongo kutegemea mahitaji kiwango kikubwa cha maji.

KIWANGO GANI CHA MAJI NI HATARI, KIASI GANI NI KINGI?

Maji mengi yanakufanya utokwe na jasho jingi, Profesa Whiteley, mtaalamu wa matatizo ya kutokwa jasho kipita kiasi anaamini kuwa kutokwa sana na maji mwilini ni sababu ya kunywa maji mengi jambo ambalo limekuwa likiwasumbua watu wengi, baadhi hali ni mbaya kufikia kiwango cha kufanyiwa upasuaji ili kuondoa mishipa inayosaidia mwili kutoa jasho.

“Kati ya mambo ambayo huwa nawauliza wagonjwa wangu ni kwa kiasi gani wanakunywa” anasema “wao hunijibu hunywa maji mengi kufidia jasho jingi wanalotokwa. Huwa wanashangaa ninapowaambia tabia zao za kunywa maji mengi ndio chanzo cha kutokwa jasho jingi. Jasho ni njia moja ambayo mwili hutumia kutoa maji isiyoyahitaji. Wagonjwa wengi hugundua kiwango cha kutokwa jasho hupungua baada tu ya kupunguza unywaji maji mengi” – Profesa Whitley

SHIDA YA KUPATA USINGIZI

Kunywa maji mengi, hasa nyakati za jioni huleta usumbufu wakati wa kulala, “tukilala ubongo wetu unazalisha homoni zinazo shusha utendaji kazi wa ini ili kupunguza hisia za kubanwa na haja ndogo nyakati za usiku.” Anasema Profesa Whitley.

Anasema kama unakunywa glasi mbili au tatu jioni, maji yote yasiyohitajika yanatafuta njia ya kutoka mwilini, hivyo kuathiri homoni za kupunguza kasi ya ini na kujaza kibofu cha mkojo, jambo ambalo linakulazimu kukatisha usingizi wako ili uende chooni na kuwa shida kupata tena usingizi.

Mtaalam anashauri kutokunywa maji masaa mawili au hata matatu ni vizuri zaidi kabla ya kulala, pia kuoga maji ya uvuguvugu kabla ya kwenda kulala, ili utokwe jasho kiasi wakati unalala, hivyo hautosumbuka sana kubwana na haja ndogo wakati umelala.


KIFO KWA SUMU YA MAJI

Mwaka 2008, mama wa miaka 40, Jacqueline Henson, aliyekuwa katika program ya kupunguza uzito, alipoteza maisha sababu ya sumu ya maji iliyosababishwa na kunywa lita 4 za maji kwa muda mfupi.

Pamekuwa na shuhuda kadhaa za madhara ya kunywa maji mengi kupita kiasi. “Kunywa maji mengi haraka, huleta shida na haswa uwiano wa chumvi mwilini” anaeleza Dkt Frankie Phillips mtaalam wa chakula kutoka Uingereza.

Unapokunywa maji mengi kwa muda mfupi, ini linashindwa kuondoa maji yasiyohitajika haraka na damu yetu inakuwa nyepesi yenye majimaji kuliko inavyotakiwa na kusababisha kuwa na upungufu wa chumvi.

‘Kwa kawaida viwango vya chumvi katika seli na damu viko sawa. Lakini inapotokea damu inapungukiwa chumvi yaweza kusababisha seli fulani katika ubongo kuvimba. Hiyo yaweza kusababisha shinikizo(preasure) katika fuvu na kusababisha kuumwa kichwa na wakati mwingine kufikia kusababisha sumu ya maji jambo ambalo ni hatari’


MAJI KIASI GANI YANAHITAJIKA MWILINI KWA SIKU?

Wataalam wa kuondoa sumu mwilini, waalimu wa mazoezi, na wataalamu wa chakula wanashauri tunywe japo lita 2 za maji kwa siku – wakati mwingine hata mpaka lita 4 – lakini kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, wataalam wanashauri mwanamke mtu mzima anahitaji japo lita 1.6 za vimiminika mwilini (sio maji peke yake) kwa siku. Wanaume ni lita 2 kwa siku ili mwili ufanye kazi vizuri.

Vimiminika hivyo ni vinywaji ambayo vinakubalika ikiwa ni pamoja na vya moto kama chai, kahawa, maziwa na hata juisi za matunda, hata maji yaliyopo katika matunda na mboga za majani.

David Wheeler, Mtaalamu wa magonjwa ya ini, ambaye pia ni msemaji wa tafiti za magonjwa ya ini nchini Uingereza, anasema ‘huitaji kunywa maji ili kutokwa jasho, haja ndogo na kulifanyisha kazi kubwa ini. Vimiminika vyote ni sawa mwilini, tofauti iko kwenye pombe ambayo ina kemikali inayolewesha na hufanya mwili kuishiwa maji.’

Mtaalamu wa chakula Dr Frankie Phillips anakubali. ‘Maji ni mazuri mwilini sababu husafisha mwili bila kuongeza kalori unapokunywa’ anasema unapochanganya vinywaji siku nzima – mfano maziwa (kuna madini ya chokaa mengi), juisi ya matunda (vitamin C) inatosha kama unahitaji virutubisho muhimu mwilini.

“ni vyema kujitahidi kuachana na vinywaji vyenye makemikali, ambavyo huchanganywa na sukari, kwani ni hatari kwa mwili wako na meno”


UTAJUAJE UMWKUNYWA VYA KUTOSHA?


Viwango vya unywaji maji hutofautiana na ukubwa na maumbile yetu, jinsi tunavyojishughulisha na mazingira tuliyopo. Pia utahitaji maji mengi kutokana na hali ya hewa, kama uko maeneo ya joto.

Njia pekee ya kujua kama mwili unahitaji maji ni kwa kusikilizia kiu. Kama una kiu utahitaji kunywa maji. Pia unaweza kujua mahitaji yako kwa kuangalia rangi ya mkojo wako. Rangi ya mkojo inatakiwa kuwa nyeupe kiasi. Mkojo unavyozidi kuwa mweusi ndivyo unavyohitaji kunywa maji zaidi. Kama utakuwa na rangi nyeupe kama maji maana yeke ni kwamba umekunywa maji mengi hivyo inabidi upunguze.



No comments:

Post a Comment