Tuesday, January 29, 2013

RICK ROSS ANUSURIKA KUFA



Nyota wa Hip Hop  Rick Ross, anusurika kupoteza maisha baada ya kukoswa koswa na risasi kadhaa kwenye gari yake aina ya Rolls Roys zilizorushwa na mtu mmoja ambaye bado hajafahamika

Taarifa za polisi zinasema kuwa asubuhi ya jana  wamepokea simu nyingi kutoka kwa wakazi ambao wanaishi maeneo ya Las Olas baada ya kusikia mlio wa risasi

polisi wanasema gari lingine lilisimama karibu na gari la nyota huyo  na mtu mmoja aliekuwa ndani ya gari hilo kuanza kurusha risasi kwenye gari la Ross

Nyota huyo  hakupatwa na risasi hata moja wakati wa tukio hilo na hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa ndani ya gari hilo.

Mpaka sasa hakuna alietuhumiwa, kugundulika wala kushikiliwa juu ya tukio hilo, polisi wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo



ALICIA KEYS AFUNIKA



 Mwanamuziki Alicia Keys wikiendi iliyopita alitua Kusini mwa Ufaransa kwa ajili ya kuhudhuria tuzo za muziki za NRJ. Mwanadada huyo alikuwa ametokelezea katika vazi la gauni lililobuniwa na Michael Kors na aliongozana na mume wake Swizz Beatz






BEYONCE AUMBUKA




Imekuwa ni wiki ya hekaheka kwa mwanamuziki mwenye makazi yake Texas, Beyonce. Mwanamuziki huyo alijikuta akidhalilika baada ya kugundulika kuwa hukufanya 'Live'shoo

Onyesho hilo lilikuwa rekodedi , huku kila shabiki wake  alidhani kuwa Beyonce amefanya shoo nzuri kabla ya kugundua kuwa shoo hiyo ilikuwa ya kurekodiwa, kitu ambacho kiliwafanya kulalamika

Mwanamuziki Kelly Clarkson aliyepanda kabla ya Beyonce alicheza miziki yake 'Live'

Taarifa hizo zimekuja wakati mbaya kwa Beyonce kwa kuwa mwanamuziki huyo amekuwa katika jitihada la kujiunga tena na kundi la Destiny Child huku kukiwa na tetesi kibao kuhusiana na uhusiano na mume wake pamoja na mtoto wake


Thursday, January 24, 2013

NYOTA WA DESTINY CHILD AFUNGUKA


Nyota wa kundi la Destiny Child, Michelle Williams amefunguka kuhusiana na vita aliyekuwa nayo dhidi ya sononi ili kusaidia wengine wanaokabiliwa na tatizo hilo

Muimbaji huyo kwanza alipata wakati mgumu akiwa mtoto kutokana na maisha duni, alisema amekuwa akipambana na giza kwa miaka kadhaa

Lakini nyota huyo ambaye hivi karibuni ameungana na wanamuziki wenzake wanaounda kundi la Destiny akiwemo Beyonce na Kelly Rowland alisema sasa mambo yanaenda vizuri

Muimbaji huyo mwenye hofu ya mungu sasa anakusudia kutoa ushauri kwa wanawake wanaokabiliwa na matatizo "Tuna nguvu jaribu kusali na kwenda kanisani kuhusiana na shida yako mungu atakuponya"


Tuesday, January 22, 2013

WIZ KHALIFA NA AMBER ROSE WAJIANDAA KUPATA MTOTO


Amber Rose na Wiz Khalifa wanahesabu siku zote hadi mtoto wa kiume atakapozaliwa siku mbili kabla ya kwenda darasa la mafunzo ya uzazi

BEYONCE AIMBA WIMBO WA TAIFA KATIKA SHEREHE ZA KUAPISHWA BARAKA OBAMA




Beyonce Knowles alifanya kitu cha tofauti Washington DC kwa kuingia katika historia ya aina yake kwa kuimba nyimbo ya taifa ya nchi hiyo siku ya sherehe za kuapishwa kwa rais Baraka Obama

Beyonce aliongozana na  mumewe Jay Z, siku ya sherehe hiyo


Monday, January 21, 2013

DEELISHIS AONGEZA TATOO KATIKA MAKALIO YAKE

 Nyota Deelishis ameamua kuongeza umakini katika sehemu zake za nyuma ya mwili wake , kama hiyo haitoshi pia nyota huyo ameongeza umakini kwa kuamua kujiongeza michoro zaidi katika sehemu zake za nyuma ya mwili wake na kutokea katika cover la magazine la Straight Stunt ambapo aliongeza baadhi ya kazi za sanaa za wasanii maarufu



Friday, January 11, 2013

NELLY KATANGAZA KUACHANA RASMI NA ASHANTI, SASA KUTOKA NA KIMWANA MWINGINE



Wakati mapenzi ya mwanamuziki Nelly na Ashanti yakionekana kuanza kurudi katika njia, wawili hao wametangaza rasmi kuachana baada ya kuwa wapenzi kwa muda wa miaka tisa.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Nelly sasa anatoka na model na muigizaji Tae Heckard, huku Tae mwenyewe kwa namna moja au nyingine akithibitisha tetesi hizo baada ya kuweka picha yake akiwa na Nelly katika mtandao wa Instegram

Nelly na Tae siku zote wamekuwa marafiki wakubwa Kwa mara ya kwanza walikutana miaka kumi iliyopita na toka hapo wakawa marafiki huku wakitoka mara kwa mara.

Tae amejipatia umaarufu kutokana na jukumu lake katika BET's The Game, na pia katika toni za video za muziki. Video ya hivi karibuni ambayo Tae alionekana ni ile ya Keyshia Cole 'Trust & believe'. Muigizaji huyo pia amewahi kutokea katika video ya nyimbo ya Nelly ya mwaka 2006 inayoitwa 'Grillz'



Friday, January 04, 2013

WAOMBOLEZAJI

Mke wa marehemu Sajuki aliyejifunika nguo nyeupe akizungukwa na baadhi ya ndugu wakimfariji kutokana na kufiwa na mumewe, Sajuki anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam



MAELFU KUMZIKA SAJUKI LEO

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) akiteta jambo na msanii mwenzie 



Baba wa marehemu Sajuki akiwa anabadilishana mawazo na baadhi ya wasanii nyumbani kwa marehemu Tabata