Tuesday, January 29, 2013

RICK ROSS ANUSURIKA KUFA



Nyota wa Hip Hop  Rick Ross, anusurika kupoteza maisha baada ya kukoswa koswa na risasi kadhaa kwenye gari yake aina ya Rolls Roys zilizorushwa na mtu mmoja ambaye bado hajafahamika

Taarifa za polisi zinasema kuwa asubuhi ya jana  wamepokea simu nyingi kutoka kwa wakazi ambao wanaishi maeneo ya Las Olas baada ya kusikia mlio wa risasi

polisi wanasema gari lingine lilisimama karibu na gari la nyota huyo  na mtu mmoja aliekuwa ndani ya gari hilo kuanza kurusha risasi kwenye gari la Ross

Nyota huyo  hakupatwa na risasi hata moja wakati wa tukio hilo na hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa ndani ya gari hilo.

Mpaka sasa hakuna alietuhumiwa, kugundulika wala kushikiliwa juu ya tukio hilo, polisi wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo



No comments:

Post a Comment