Friday, January 11, 2013

NELLY KATANGAZA KUACHANA RASMI NA ASHANTI, SASA KUTOKA NA KIMWANA MWINGINE



Wakati mapenzi ya mwanamuziki Nelly na Ashanti yakionekana kuanza kurudi katika njia, wawili hao wametangaza rasmi kuachana baada ya kuwa wapenzi kwa muda wa miaka tisa.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Nelly sasa anatoka na model na muigizaji Tae Heckard, huku Tae mwenyewe kwa namna moja au nyingine akithibitisha tetesi hizo baada ya kuweka picha yake akiwa na Nelly katika mtandao wa Instegram

Nelly na Tae siku zote wamekuwa marafiki wakubwa Kwa mara ya kwanza walikutana miaka kumi iliyopita na toka hapo wakawa marafiki huku wakitoka mara kwa mara.

Tae amejipatia umaarufu kutokana na jukumu lake katika BET's The Game, na pia katika toni za video za muziki. Video ya hivi karibuni ambayo Tae alionekana ni ile ya Keyshia Cole 'Trust & believe'. Muigizaji huyo pia amewahi kutokea katika video ya nyimbo ya Nelly ya mwaka 2006 inayoitwa 'Grillz'



No comments:

Post a Comment